MOJA KWA MOJA: MATOKEO YA UCHAGUZI UGANDA
10:37 Kiongozi wa waangalizi wa IGAD Yufnalis Okubo asema kwa
maoni ya kundi lake la waangalizi, uchaguzi ulitimiza viwango vinavyohitajika
kimataifa. Ahimiza walioshiriki kukubali matokeo. Awataka wasioridhika kutumia
mifumo ya sheria kulalamika.
10:30 Kiongozi wa waangalizi wa IGAD Yufnalis Okubo anasema
kulikuwa na changamoto katika kuandaa vituokwa upigaji kura pamoja na
kufunguliwa kwa vituo. Asema pia waliona mabango ya kampeni katika baadhi ya
vituo vya kupigia kura. Asema siku ya uchaguzi, baadhi ya wapiga kura walikosa
majina yao vituoni. Wasiojua kusoma hawakusaidia vyema. Waliofaa kupaka watu
wino baada ya kupiga kura katika baadhi ya maeneo hawakumakinika sana.
Apendekeza vifaa vya kupigia kura viwe vikifikishwa mkesha wa siku ya kupiga
kura, sawa na kuandaliwa kwa vituo.
10:25 Kiongozi wa waangalizi wa COMESA Ashraf Gamaal Rashed
amesema Tume ya Uchaguzi inafaa kuwezeshwa zaidi ili kutekeleza majukumu yake
vyema.
10:20 Waangalizi wa uchaguzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,
COMESA na IGAD wanatoa taarifa zao kuhusu uchaguzi. Rais wa zamani wa Tanzania
Ali Hassan Mwinyi amewapongeza wananchi wa Uganda kwa kujitokeza kwa wingi.
Amesema uchaguzi ulifiofanyika wiki hii ulikuwa na ushindani mkubwa.
09:59 Ubalozi wa Marekani nchini Uganda umekanusha taarifa ambazo
zimekuwa zikisambazwa mitandaoni zikiashiria kwamba Marekani imewaagiza raia
wake waondoke Uganda. Ubalozi huo umesema taarifa hizo ni za uongo.
08:44 Bw Kiggundu amesema matokeo mengine yanatarajiwa mwendo wa
saa nne, lakini yanaweza yakatangazwa mapema iwapo yatakuwa tayari. Ametetea
tume hiyo dhidi ya madai kwamba kura kutoka 'ngome za upinzani' hayajaripotiwa.
Tume inatarajiwa kutangaza matokeo kamili kabla ya saa kumi alasiri kwa mujibu
wa sheria.
08:38 Matokeo yaliyotangazwa sasa hivi ni kama ifuatavyo. Ni
kutoka vituo 21,254 kutoka kwa vituo 28,010. Matokeo yaliyotangazwa
yanajumuisha kura 7,822,737 ambazo ni sawa na asilimia 51,21 ya wapiga kura 15
milioni waliosajiliwa na tume hiyo. Kumbuka si wapiga kura wote waliosajiliwa
ambao hufanikiwa kupiga kura.
|
Matokeo
kwa sasa (Vituo 21,254 kati ya 28,010)
|
||
|
Abed Bwanika
|
70,708
|
0.95%
|
|
Amama Mbabazi
|
112,071
|
1.50%
|
|
Baryamureeba Venasius
|
42,931
|
0.58%
|
|
Benon Biraaro
|
20,553
|
0.28%
|
|
Kizza Besigye
|
2,603,880
|
34.94%
|
|
Joseph Mabirizi
|
19,661
|
0.26%
|
|
Maureen Kyalya
|
32,773
|
0.44%
|
|
Yoweri Museveni
|
4,549,148
|
61.05%
|
|
Chanzo: Tume ya Uchaguzi Uganda (EC)
|
||
08:33 Mwenyekiti wa EC Badru Kiggundu anaanza kutangaza matokeo ya
karibuni zaidi.
08:32 Kwa sasa ni wakati wa maombi Namboole, kabla ya kutangazwa
kwa matokeo ya kwanza ya urais ya karibuni zaidi leo.
08:28 Katibu Mkuu wa chama tawala cha NRM Justine Kasule Lumumba
amekuwa akiwahutubia wanahabari kutoka Bweyogerere
Museveni anaongoza. NRM inaongoza
katika kura za urais na za ubunge na tunasubiri matokeo ya mwisho. Hata kule
mawaziri wameshindwa, ni watu wa kawaida. Waganda waliamua nani anafaa
kuwaongoza. Kwa NRM si habari njema, lakini ni lazima tukubali.
08:13 Waangalizi wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kuhutubia
wanahabari kuhusu uchaguzi mkuu wa Uganda saa sita kasorobo.
08:10 Mwenyekiti wa EC Badru Kiggundu ameingia ukumbini kutangaza
matokeo ya karibuni zaidi ya uchaguzi.
07:54 Tume ya taifa ya uchaguzi Uganda inatarajiwa kutoa matokeo
mengine mwendo wa saa mbili asubuhi.
07: 52 Matokeo yaliyotangazwa kufikia sasa ni kama ifuatavyo:
|
Matokeo
kwa sasa (Vituo 15,799 kati ya 28,010)
|
|
|
Abed Bwanika
|
51,150
|
|
Amama Mbabazi
|
88,900
|
|
Baryamureeba Venasius
|
33,135
|
|
Benon Biraaro
|
15,588
|
|
Kizza Besigye
|
1,767,041
|
|
Joseph Mabirizi
|
14,757
|
|
Maureen Kyalya
|
24,536
|
|
Yoweri Museveni
|
3,156,070
|
|
Chanzo: Tume ya Uchaguzi Uganda (EC)
|
|
07:50 (Saa za Afrika Mashariki) Hujambo! Twatumai umeamka salama.
Karibu kwa taarifa za moja kwa moja kuhusu uchaguzi mkuu wa Uganda. Matokeo ya
uchaguzi wa urais uliofanyika Alhamisi nchini Uganda yanaendelea kutangazwa,
matokeo kamili yakitarajiwa kutolewa baadaye leo alasiri.
habari kutoka BBCswahili
Tanzanian Shilling Converter
No comments: