POLISI MKOANI MARA YAWAKAMATA WATU SABA KWA KUBAKA NA MAUAJI YA MTOTO.

Jeshi
la Polisi mkoani Mara linawashikilia watu saba kwa tuhuma za kumbaka
kisha kunyongwa hadi kufa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne na
nusu Mariam Deaogratus ambaye aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya awali ya
makoko katika manispaa ya Musoma.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mara kamishna msaidizi wa jeshi la polisi
ACP Philip Alex Kalangi, amesema watu hao wamekamatwa siku moja tu
baada ya kutokea kwa tukio hilo la kikatili.
Awali kamanda alisema mtoto huyo alikumbwa na mkasa huo muda mfupi
baada ya kuondoka nyumbani kwao jioni ya Februari 23 mwaka huu kwenda
shule kwa ajili ya masoma ya ziada, lakini akuonekana tena hadi saa 2
usiku wa siku hiyo Februari 23, mwili wake ulipokutwa ametupwa katika
nyumba ambayo ujenzi wake unaendelea.
Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama
wilaya ya Musoma, kamishina mwandamizi mstaafu wa jeshi la polisi Zeloth
Stephen, amesema vyombo vya dola vitafanya kila Nnjia katika
kuhakikisha mtu yoyote ambaye amefanya kitendo hicho cha kikatili
anakamatwa na kufikishwa mara moja katika vyombo vya sheria.
No comments: