WAZALISHAJI SUKARI WADAI USAMBAZAJI SUKARI UNAHUJUMIWA NA KUTENGEZA UHABA.
Sakata
la kupanda bei ya sukari limechukua sura mpya baada ya umoja
wazalishaji wa Sukari kudai kuwa kuna njama za baadhi ya wafanyabiashara
wakubwa ambao mianya yao ya uingizaji wa sukari kutoka nje ya nchi
imezibwa hivyo wameanza kuhujumu sukari ya ndani.
Mwenyekiti wa umoja wa wazalishaji hao wa sukari balozi Ami Mpungwe
amesema wana uhakika njama za wafanyabiashara hao hazitafanikiwa kwani
bei halisi ya Sukari ambayo inapaswa kuuzwa kwa rejareja haitakiwi
kuzidi elfu mbili kwa kilo moja.
Naye kaimu mkurugenzi mkuu wa bodi ya Sukari Abdul Mwankemwa
amesema kuna wafanyabiashara ambao wamehodhi sukari katika maghala kwa
lengo la kuifanya iwe adimu na hivyo bei yake kupanda.
Kuhusiana na kwanini bei ya sukari kutoka nje ya nchi kuuzwa kwa
bei nafuu kuliko ile inayozalishwa ndani ya nchi mmoja wa wazalishaji
hao wa Sukari Seif Ali Seif kutoka kiwanda cha Sukari Kagera anaeleza.
No comments: