MAWAZIRI AMBAO HAWAJAJAZA FOMU ZA MAADILI WAPEWA SAA 12 KUJAZA FOMU HIZO.

Saa
chache tangu waziri mkuu Mh Kassim Majaliwa atangaze majina ya mawaziri
wanne na naibu waziri mmoja kuwa wanatakiwa kuwasilisha fomu zao za
maadili ya utumishi ya ummaa na mali wanazomiliki katika ofisi ya tume
ya taifa ya maadili la sivyo watakuwa mawejionda wenyewe katika nafasi
zao waziri wa mambo ya ndani Mh Charles Kitwanga ambaye ni mmoja ya
mawaziri waliotajwa amesema amesikitihwa sana na kitendo cha kutajwa
jina lake kuwa hajarudisha fomu zake wakati amekwisha fanya hivyo muda
mrefu.
Akizungumza na waandishia wa habari Mh Majaliwa amesem ameagizwa na
rais John Magufuli kuwa wale wote mabo wamekiuka sheria na kuacha
kujaza na kurudisha fomu hizo awataje na kisha watekeleze agizo hilo
ndani ya saa kumi na mbili.
Hata hivyo baada ya kutolewa kwa tangazo hilo ITV ilipiga kambi
katika ofisi za tume ya maadili kwa lengo la kuweza kubaini kama kuna
waziri ambaye ataitikia agizo hilo na ndipo ilipofika saa 6:45 alikuja
Mh Kitwanga ambaye alisema ameshangaa kuona jina lake limetajwa na hivyo
anakwenda katika ofisi za tume hiyo kutoa malalamiko yake.
Ilipofika saa 7:05 mchana naye waziri wa mambo ya nje, ushirikiano
wa Afrika Mashariki, kikanda na kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine
Mahiga ambaye alikiri kutorudisha fomu hizo kutokna na kuwa na majukumu
mengi.
Kabla ya kwenda katika ofisi za tume kituo hiki kilikwenda katika
ofisi za naibu waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais mazingira na
muungano Mh Luhaga Mpina saa 5:30 ambaye hakunonekana kuwa na taarifa za
agizo la waziri mkuu na baada ya kupewa taarifa na mwandishi akakiri
kurudisha fomu hizo kwa sababu alipoteuliwa hakuwa anajuwa mshahara wake
na stahiki zingine lakini sasa anajuwa ataipeleka.
chanzo ITV
No comments: