TUKIO LA UJAMBAZI MBAGALA WATU SABA WAMEUAWA AKIWEMO ASKARI POLISI MMOJA,ASKARI BINAFSI WAWILI NA RAIA JIJINI DAR ES SALAAM.

Watu
saba wakiwemo majambazi watatu wameuawa baada ya kutokea kurushiana
risasi kati ya majambazi na Polisi kabla na baada ya majambazi hao
kuvamia tawi la Access Benki lililopo Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es
Salaam.
Kamanda wa Polisi katika kanda maalum ya dar es salaam kamishina
simon siro amesema majambazi 12 wakiwa katika pikipiki sita walivamia
benki hiyo kwa nia ya kuiba fedha jaribio ambalo kwa kiasi kikubwa
halikufanikiwa.
Amesema mbali ya majambazi watatu kuuawa,pia Polisi mmoja,askari wa
kampuni binafsi ya ulinzi na raia wawili nao waliuawa katika tukio hilo
ambapo majambazi walizitelekeza pikipiki zao na kuchanganyika na raia
na baadaye kudaiwa wamekimbilia katika msitu wa Kongowe unaotenganisha
mkoa wa DSM na Pwani.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Charles Kitwanga amesema mara
baada ya mkutano huo na waandishi wa habari atawasiliana na waziri wa
ulinzi ili wapatikane askari kutoka JWTZ kusaidia msako wa majambazi
ambao wanadaiwa kujificha katika misitu inayotenganisha mikoa hiyo
miwili.
Nao waendesha pikipiki wametakiwa kuwa wavumilivu kwani kuanzia
sasa msako maalum unaendelea kuwabaini wahalifu ambao wengi wao hutumia
Pikipiki.
No comments: