UMOJA WA AFRIKA UMETANGAZA KWAMBA UTAWAPELEKA WAANGALIZI 100 WA HAKI ZA KIBINAADAMU PAMOJA NA WAANGALIZI WENGINE 100 WA KIJESHI NCHINI BURUNDI


Jazob Zuma
Umoja wa Afrika umetangaza kwamba utawapeleka waangalizi 100 wa haki za
kibinaadamu pamoja na waangalizi wengine 100 wa kijeshi nchini Burundi.
Umesema kuwa rais wa taifa hilo Pierre Nkurunziza ameunga mkono mpango huo.
Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma aliongoza ujumbe wa viongozi watano wa Afrika katika ziara ya siku mbili wiki hii.
Walikutana na bwana Nkurunziza na viongozi wawili wa upinzani ambao
wamesalia nchini humo hata baada ya ghasia zilizozuka mwezi Aprili baada
ya Nkurunziza kutangaza kuwa atawania muhula wa tatu.
Wamesema kuwa mpatanishi wa AU rais Museveni wa Uganda ataanzisha mazungumzo hivi karibuni.
habari kutoka BBCswahili
habari kutoka BBCswahili
No comments: