Ads Top

WAZIRI WA UJENZI PROF. MBARAWA AWAONYA WATUMISHI WA TTCL WASIO WAAMINIFU MWANZA.

Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mh. Prof. Makame Mbarawa amewaonya vikali baadhi ya watumishi wa kampuni ya simu Tanzania ( TTCL ), wanaojifanya kuwa mawakala wa kampuni nyingine za simu kuacha mara moja tabia hiyo, la sivyo atawafukuza kazi kwani ni heri kampuni ikabaki na watumishi wachache waadilifu kuliko kuwa na wafanyakazi wengi wasio waaminifu wanaoendelea kuihujumu TTCL.


Prof. Mbarawa ametoa onyo hilo baada ya kutembelea na kujionea hatua za ujenzi wa mradi wa upanuzi wa mkongo wa taifa awamu ya tatu katika vituo vya Ghana na Mwanza telephone house eneo la posta jijini Mwanza. 

Meneja wa TTCL mkoa wa Mwanza Johnbosco Kalisa kilio chake ni madeni ya wateja sugu zikiwemo idara za serikali.

Baadhi ya wafanyakazi wa TTCL na posta mkoani Mwanza wanaeleza kilio chao kwa waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mh. Prof. Makame Mbarawa juu ya changamoto wanazokumbana nazo katika utendaji wao wa kazi za siku kwa siku.
Pamoja na TTCL kupewa jukumu la kuongoza mkongo wa taifa kwa kutumia teknolojia ya Optical Fibre, ambapo Mwanza ni kiungo kikuu cha kanda ya ziwa na nchi jirani, ulinzi na usalama wa mkongo huo bado unakabiliwa na hujuma zinazodaiwa kufanywa kwa makusudi na baadhi ya watu pamoja na wakandarasi wa barabara wanapokuwa kazini.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.