VIGOGO WANNE WA MSD WASIMAMISHWA KAZI KWA UBADHILIFU WA SHILINGI BILIONI 1.5.
Serikali imewasimamisha kazi vigogo wanne wa bohari kuu ya dawa MSD kwa tuhuma za ubadhilifu wa shilingi bilioni moja na nusu kwa kukiuka taratibu za manunuzi.
Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mh Ummy
Mwalimu amewataja maafisa hao waliosimamishwa kuwa ni mkurugenzi wa
kanda huduma za wateja Cosmas Mwaifwan, mkurugenzi wa fedha Joseph
Tesha, mkurugenzi wa ugavi Misanga Muja na Henry Mchunga, mkurugenzi wa
manunuzi.
Mh Mwalimu ametoa taarifa hiyo alipokuwa akipokea vitanda zaidi ya
100 kutoka MSD zoezi lililoambatana na kuvifunga katika wodi mpya ikiwa
ni utekelezaji wa agizo la rais John Magufuli alipotembelea wodi ya
wazazi hivi karibuni na kukuta wakiwa wamelala chini.
Katibu mkuu wa wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na
watoto Mpoki Ulisubisya akizungumza wakati wa ufungaji wa vitanda hivyo
amesema jengo hilo lina uwezo wa kulaza kina mama 120 na kuhusu
watumishi wa wizara yake waliokuwa wanatumia jengo hilo amesema.
Baadhi ya kina mama ambao walikuwa wanakabiliwa na kero ya kulala
chini na ambao wamepata nafasi ya kuhamia jengo jipya mbali na
kumshukuru rais Magufuli wamesema.
Wakati huohuo Mh Ummy ametangaza mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu
kuwa umerudi tena jijini Dar es Salaam ambapo wagonjwa sita kutoka
wilaya ya Temeke wamegunduliwa huku mikoa 11 ikiripotiwa kuwa na
wagonjwa wapya na mkoa wa Iringa ukiongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya
wagonjwa ambao ni 199.
chanzo ITV
chanzo ITV
No comments: