Ads Top

WAZIRI WA UJENZI PROF MBARAWA AMSIMAMISHA KAZI MENEJA WA FEDHA WA ATCL.

Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Prof Makame Mbarawa amemsimamisha kazi meneja wa fedha wa shirika la ndege Tanzania ATCL Bw. Steven Kasubi kufuatia upotevu wa fedha zaidi ya sh. milioni mia saba ambazo zilitokana na uuzwaji wa tiketi za ndege.

Waziri Mbarawa ametoa taarifa hiyo jijini Dar es Salaam ambapo amesema wizi huo umefanywa kwa kushirikiana na wafanyakazi wa shirika hilo kupitia kampuni ya wakala wa ukatishaji tiketi ya salama World Travel iliyopo visiwa vya komoro.

Aidha amesema amemwagiza mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kufanya uchunguzi kwa mawakala wengine wote wa shirika hilo kubaini kama fedha za uuzaji wa tiketi hizo zinarudishwa kama inavyotakiwa.

Wakati huohuo waziri Mbarawa amekutana na sekta binafsi ili kujadili kwa pamoja changamoto zinazoikabili na namna ya kuzitatua.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.