EWURA YATANGAZA BEI ELEKEZI YA NISHATI YA MAFUTA NCHINI.

Bei
ya nishati ya mafuta imeendelea kushuka baada ya mamlaka ya udhibiti wa
huduma za nishati na maji EWURA kutangaza bei kikomo huku baadhi ya
wananchi wakitaka bei za bidhaa nazo zishuke.
Akitangaza bei elekezi jijini Dar es Salaam mkurugenzi mkuu wa
EWURA Bw.Felix Ngamlagosi amewataka wateja wa nishati ya mafuta kudai
risiti pindi wanapopewa huduma hiyo na kwamba kuanzia sasa wananchi
wanaweza kupata bei hizo kupitia simu zao za kiganjani.
Baadhi ya wananchi wameeleza kushangazwa na kitendo cha nishati
hiyo kushuka mara kadhaa lakini bei za bidhaa kuendelea kupanda na
kuitaka serikali kuunda tume ya bei huku wauzaji wa nishati hiyo
wakielezea changamoto wanachokabiliana nazo katika kutoa risiti kwa
wateja.
No comments: