TANESCO YADHAMIRIA KUFUTA GHARAMA ZA HUDUMA KWA WATEJA (SERVICE CHARGE).
Wakati nchi kwa sasa ikiwa mguu sawa kuelekea kwenye kipato cha
kati yenye uchumi wa viwanda, nishati ya umeme wa uhakika ndiyo
inayoweza kutimiza ndoto hiyo ya nchi, lakini TANESCO wanasema
wamejipanga vema kimfumo tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Miongoni mwa mipango mikuu ya kurahisha huduma ya utaoji wa
nishati hiyo ya umeme,ni pendekezo la kufutwa kwa gharama za huduma kwa
wateja, yaani SERVICE CHARGE,huku tatizo la baadhi ya vituo vya kuuzia
umeme kushindwa kutoa huduma ipasavyo nalo likiwa tayari limekwisha
kushughulikiwa.
Afisa huyo mwandamizi wa TANESCO makao makuu amewatoa hofu
watanzania kuhusu nishati hiyo huku akisema ni lazima ya shirika hilo
kuona ndoto ya tanzania yenye viwanda inatimia ikiwa na umeme wa
uhakika.
Wananchi wanasema mipango ya uondoaji wa gharama za huduma kwa
wateja ni neema kwao kwani itawaondolea gharama nyingi walizokuwa
wakitumia kununua umeme.
No comments: