NIDA KUTOA TAREHE RASMI YA UCHUKUAJI VITAMBULISHO VYENYE SAINI
Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa nchini Tanzania (NIDA) imekiri kwamba
vitambulisho vya taifa vilivyogawiwa havina saini pande zote za nje na
na hivyo itautangazia umma tarehe rasmi ya kuanza kutolewa kwa
Vitambulisho vilivyofanyiwa maboresho na maelekezo kuhusu Vitambulisho
visivyo na saini ambavyo vimekwisha gawiwa.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na kitengo cha
Mawasiliano na Hifadhi Hati Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)
kwaajili ya kuwataarifu wananchi na wadau ni kwamba vitambulisho vya
Taifa vitakuwa na Saini ya Mmiliki wa Kitambulisho mbele ya Kitambulisho
na Mamlaka ya Kutoa Vitambulisho vya Taifa (Mkurugenzi Mkuu) nyuma ya
Kitambulisho.
Taarifa hiyo imesema kuwa mamlaka hiyo kwa sasa inafanya jitihada
za kurekebisha kanuni, utaratibu na muundo wa Vitambulisho ili kukidhi
mahitaji ya wadau.
Hata hivyo kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imesema kuwa kuweka saini juu ya
Vitambulisho vya Taifa kunawezesha utambuzi na uthibitishaji wa taarifa
za mmiliki wa Kitambulisho cha Taifa ambao haulazimu kutumia alama za
vidole.
Vilevile NIDA imewashukuru wadau wote kwa maoni yao hususani suala
la kuweka saini juu ya Vitambulisho vya Taifa ili kurahisisha utambuzi
wa mmiliki wa Kitambulisho na matumizi mengine ambayo tumeona ni budi
kuyafanyia marekebisho.
Aidhaa wadau wote wa NIDA ambao wana vifaa maalumu vya kusoma
taarifa zilizomo kwenye Kitambulisho (Card Readers) na ambao
wameunganisha mifumo yao na Mfumo wa Usajili na Utambuzi wa Watu
wataendelea kutumia njia hizo kuthibitisha taarifa na utambuzi wa watu.
No comments: