Kitwanga: Hata nikijamba Ushuzi Mtaandika.
Na mwandishi wetu Antony Sollo Misungwi.
MBUNGE wa jimbo la Misungwi Charles Kitwanga amesema
kuwa kwa sasa hahitaji kuongea chochote na waandishi wa Habari maana ni wambea
kwani hata akijamba ushuzi wataandika.
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo sept 15 majira ya saa
2: 30 nyumbani kwake Usagara baada ya waandishi kufika nyumbani hapo kufuatia
mwaliko wa kukutana naye kwa lengo la kutolea ufafanuzi masuala mbalimbali ikiwemo
kero ya maji inayowatesa wananchi wa Usagara na vitongoji vyake kufuatia
kupanda kwa bei ya maji na kufikia shilingi 500 kwa ndoo ya lita 20 na hata
hivyo hayapatikani.
Baada ya waandishi hao kufika tu na kuonana na
Kitwanga waliambulia maneno hayo ambapo
alisema hahitaji kuongea jambo lolote kwa kuwa waandishi wamekuwa
wakiandika umbea dhidi yake.
Walipomkumbusha kuwa kulikuwa na ahadi ya kukutana
kwa ajiri ya kutolea ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo Kitwanga
alisema aliona atoe ahadi hiyo jana kuepusha maswali toka kwa mwandishi
aliyempigia simu kupata majibu ya maswali aliyoulizwa.
“Nilikuwa na watu kwenye gari nikaona nirahisishe
tusiendelee kupoteza muda ila nasema sihitaji kuongea chochote na waandishi
ninyi ni wambea hamna dogo jamani aaaah sitaki rudini tu nyumbani mkaendelee na
shughuli zingine”alisema Kitwanga.
Wandishi
walitembelea miradi mbalimbali katika Kijiji cha Sanjo na kuambiwa kuwa kuna
ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma katika miradi hiyo ambayo Kitwanga ni mmoja
wa viongozi waliochangia kiasi kikubwa cha fedha kufikia mil 6 ili kukamilisha
miradi hiyo ambapo hata hivyo akionyesha
msimamo wake Kitwanga hakutaka kuzungumza chochote.
Katika
mradi uliotembelewa na waandishi hao walibaini kujengwa chini ya kiwango kwa
vyumba vitatu vya madarasa katika Shule ya Msingi Sanjo ambapo kabla ya kuhamia
kwa wanafunzi shuleni hapo tayari vyumba hivyo vimeshachakaa huku viongozi wa
Kijiji cha Sanjo wakiwaamuru wananchi kuchanga fedha kiasi cha 6500 kwa ajiri
ya ukarabati jambo ambalo huenda likaibua mgogoro mkubwa kijijini hapo.
No comments: