SERIKALI YATENGA BILIONI 515 KWA HALMASHAURI NCHINI KUFANIKISHA UTOAJI ELIMU BURE.
Serikali
kupitia wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na ufundi imetenga Bilioni
515.5 kwa halmashauri zote nchini katika kufanikisha utekelezaji wa
utoaji elimu bora kwa shule za msingi na Sekonndari,huku waziri wa
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mh.George Simbachawene
amesema serikali haitasita kuwachukulia hatua maafisa wa elimu na
wakurugenzi katika halmashauri watakaokuwa sio waadilifu katika
utekelezaji wa majukumu yao.
Akizungumza katika hafla ya utoaji wa zawadi kwa Halmashauri
zilizofanya vizuri katika sekta ya elimu hapa nchini waziri Simbachawene
amesema ni wajibu kwa maafisa elimu na wakurugenzi katika Halmashauri
kufanya kazi zao kwa weledi na kwa wakati kama ilivyokusudiwa.
Awali waziri wa Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi Mh.Dk,Joyce
Ndalichako alikabidhi zawadi kwa Halmashauri 10 zilizo fanya vizuri kati
ya 167,ambapo Halmashauri ya Mbinga imekuwa ya kwanza na kukabidhiwa
fedha kiasi cha shilingi milioni 331 wakati Halmashauri ya Makambako
ikiwa ni ya mwisho katika Halmashauri zote hapa nchi na kukabidhiwa
kiasi cha shilingi milioni 28.
No comments: