Ads Top

NDUGU WA WAFANYAKAZI WA MSCTN WAMLILIA MAGUFULI

Na antony Sollo, Mwanza

KUFUATIA Mgogoro mkubwa uliokuwa  ukifukuta kati ya wafanyakazi wa Kampuni ya Mwanza SateliteCables Television Network Limited (MSCTN ) inayotoa huduma za usambazaji wamawasiliano  ya TV katika maeneo mbalimbali Jijini Mwanza dhidi ya mwajiri wao ndugu wa wafanyakazi hao wamemuomba JPM awasaidie kwa kuingilia kati Mwana Halisi linaweza kuripoti.

Akizungumza na MwanaHalisi mmoja wa ndugu wa wafanyakazi hao amelalamikia ukiukwaji wa Sheria na Haki uliotekelezwa na mwajiri wa vijana hao huku akidai kuwa kulikuwa na ukandamizaji mkubwa wa Haki.
Imeelezwa kuwa wafanyakazi hao kabla ya kufanyiwa unyama huo Mwajiri wao aliwafungulia mashitaka polisi akiwatuhumu kufanya fujo na baadaye.

kuwataka kukabidhi funguo za Ofisi bila kuwapatia barua ya kuacha kazi jambo ambalo lilisababisha mgogoro huo kuwa mkubwa.

Wafanyakazi waliokuwa na mgogoro na mwajiri wao ni Samora Ernest,Waryoba Finias na Antony Lucas  wanadai ambapo kwa taarifa zilizothibitishwa na ndugu yao huyo ni kwamba wafanyakazi hao walikamatwa na polisi Machi 22, mwaka huu majira ya saa 2:00walipokwenda ofisini  na kisha wakafunguliwa kesi ya kufanya fujo na mwajiri wao huku wakiendelea kupewa vitisho kuwa atahakikisha kuwa iwapo hawataacha kudai haki zao atawafunga jela kwa madai kwamba yeye yuko vizuri na watendaji wa jeshi la polisi na vyombo vya Maamuzi.

Uchunguzi uliofanywa na MwanaHalisi umebaini kuwa sababu ya kufunguliwa kesi kwa vijana hao  ni kutokana na siri kubwa waliyokuwa nayo wafanyakazi hao juu ya tuhuma za Kampuni hiyo kukwepa kodi kwa muda mrefu  ambapo walilalamikia kitendo hicho kwa wafanyakazi wa Serikali Jijini Mwanza lakini Mwajiri alitumia kila njia kuhakikisha wanapotea uraiani.

Katika madai yao,wafanyakazi hao walikuwa wakilalamikia mapunjo ya mishahara na kunyimwa mkataba wa ajira bambapo baada ya kuonyesha msimamo wao walitishiwa kuwa wangebambikiwa kesi na mwajiri wao ili kupoteza ushahidi wa madai yao ambapo baada ya vitisho hivyo walipeleka malalamiko yao kwa Waziri wa Kazi Ajira  Vijana na Walemavu lakini hata baada ya mwajiri kupewa agizo na waziri hakutekeleza chochote ya kutekeleza adhima yake ambapo hadi sasa vijana hao wako Magereza wakitumikia kifungo.

MwanaHalisi lilipata kuiona nakala iliyokuwa na maelekezo yaliyotolewa na Kamishna
MwanaHalisi lilishuhudia jalada la kesi namba MW/RB/2526/17  lililofunguliwa dhidi wafanyakazi hao wakituhumiwa kufanya fujo ambapo kesi hiyo ilifunguliwa Kituo kikuu cha polisi kati Jijini Mwanza.
 
 “yote haya walifanyiwa na mwajiri ili kupoteza ushahidi kutokana  madai yao zote hizi zikiwa ni njama za makusudi ili  kuwanyamzisha,”alisema ndugu wa wafanyakazi hao.

Kampuni ya MSCTN inadaiwa kuwanyima wafanyakazi baadhi mikataba ya ajira, kuwapunja mishahara, kutowaandikisha kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii na hivyo kusababisha mgogoro ambao waliufikisha  kwa
Waziri wa Bunge, Sera, Vijana, Kazi, Ajira na walemavu ambapo Katibu Mkuu wa wizara hiyo alimwagiza Kamishna wa Idara ya Kazi mkoa wa Mwanza kufanya uchunguzi wa madai ya wafanyakazi hao nakuchukua hatua stahiki ili walipwe stahili zao.

“Kilichofanyika ni usanii , eti wafanyakazi walikuwa wanalazimishwa wakubali kusaini mikataba mipya bila kulipwa mapunjo yao ya nyuma na kwamba walikuwa wakilipwa mishahara pungufu ya kima cha chini cha mshahara wa serikali muda mrefu, baada ya malalamiko yao kuyawasilisha sehemu mbalimbali mwajiri wao aliamua kutengeneza mikataba feki na kuwalazimisha kuisaini jambo ambalo si sawa” alisema ndugu yao huyo kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini.

MwanaHalisi lilimtafuta Mkurugenzi wa Mwanza Cables Ridhiwani Kanji ambaye hata baada ya kutakiwa kueleza juu ya tuhuma hizo hakuwa tayari kukubali ambapo alikanusha tuhuma hizokuwa si za kweli na kwamba wafanyakazi hao waligoma kukaguliwa ili kubaini maendeleo ya matawi ya kampuni hiyo yaliyoko katika maeneo mbalimbali jijini Mwanza.
 
Kwa upende wake Afisa Kazi mkoani Mwanza Joshua Malongo alipotakiwa kutolea ufafanuzi suala hilo alikiri kupokea maagizo ya Katibu Mkuu Februari 2 mwaka huu na kufanya uchunguzi kama alivyoelekezwa ambapo  katika uchunguzi aliofanya alibaini kuwepo kwa ukweli katika malalamiko na madai ya wafanyakazi hao kuwa ni ya kweli na hivyo alimwandikia barua ya utekelezaji mwajiri wao.
 
“ Ni kweli nilipokea maagizo hayo na kuyafanyia kazi na tunapozungumza tayari nimemwandikia mwajiri wao barua ya utekelezaji ikiwa ni pamoja na kuwapa mikataba ya ajira na kuwalipa kiwango cha mshahara wa sh. 150,000 kwa mwezi kama agizo la Serikali linavyoelekeza ” alisema Joshua MwanaHalisi lilifanikiwa pia kupata nakala ya barua yenye kumb Na MWA/AD/M/43/5 ya 14.02.2017 ya Utekelezaji wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini na 6 na Sheria ya Taasisi za kazi na 7 ya 2004 ambapo hata hivyo gazeti hili limebaini kuwa hata baada ya kupelekewa barua hiyo mwajiri hajafanya  utekelezaji wowote.

Alipotakiwa kuzungumzia kutotekelezwa kwa maagizo ya Wizara ya Kazi Afisa Mwajiri wa MSCTN Fredrick Kilassa alisemakampuni hiyo inafanya shuguli zake kihalali licha ya kukiri kuwepo kwa mgogoro na wafanyakazi hao tangu Desemba 2016.

“Ninachokifahamu mimi uongozi wa kampuni hiyo uliamua kufanya ukaguzi wa miradi katika matawi mbalimbali ambayo yanatoa huduma lakini wafanyakazi wetu hawa waligoma kukaguliwa na ndiyo chanzo cha mgogoro wetu. Kuhusu tuhuma za kukwepa kodi na mapato ya Serikali MwanaHalisi lilifuatilia katika mamlaka ya Mapato TRA na kukutana na Afisa Elimu kwa mlipa Kodi Mkoa wa Mwanza Lutufya Mtafya ambaye pamoja na mambo mengine alisema kuwa amepokea taarifa hizi hata kabla ya gazeti hili kufika hapo.

“tumepokea malalamiko haya muda mrefu ila tuko katika harakati ya kuunda timu itakayokwenda kufanya uchunguzi, iwapo mwajiri wa Kampuni ya MSCTN anakusanya fedha kwa kutumia mashine moja ya EFD wakati ana matawi matano ni kosa na hivyo tutafanya uchunguzi ikibainika tutachukua hatua za kinidhamu dhidi yake”.alisema Mtafya.

Kufuatia njama za kuwabambikiza kesi vijana hawa hadi sasa wamehukumiwa kifungo katika gereza la Butimba jijini Mwanza ambapo wamemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli aingilie kati sakata hili ili kuwaokoa wanyonge wanaokandamizwa na waajiri wanaokiuka Sheria za nchi.


MWISHO

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.