Ads Top

WALEMAVU WALISHIKA PABAYA JESHI LA POLISI



Na Antony Sollo - DSM.

Kufuatia matumizi ya nguvu yaliyofanywa na Askari wa Jeshi la Polisi juni 16 mwaka huu, Viongozi wa Taasisi ya Haki za Binadamu na Maendeleo ya Kiuchumi kwa watu wenye ulemavu wametoa tamko rasmi huku wakilipa jeshi hilo siku saba kuwaomba radhi vinginevyo watalifikisha jeshi hilo Mahakamani wakiwatuhumu kwa makossa mbalimbali ikiwemo kuharibu mali,shambulizi na udahalilishaji kwa watu wenye ulemavu.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari wadau wa Haki za Binadamu kikiwemo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC wamelaani vikali matumizi ya nguvu iliyopitiliza yaliyofanywa na jeshi la polisi Tanzania katika zoezi la kuzuia kilichodaiwa kuwa ni maandamano ya watu wenye ulemavu katika eneo la Posta jijini Dar es salaam.

Akitoa Tamko kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC Wakili Anna Henga alisema kuwa,kundi la watu wenye ulemavu ni moja ya makundi maalumu katika jamii kundi ambalo linahitaji ulinzi mkubwa ili kuhakikisha usalama na mazingira mazuri.

‘Mbali na kuwekewa ulinzi kwa mujibu wa Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kundi hili la walemavu nchini linahitaji kuhakikishiwa usalama maana nchi yetu imeingia mikataba ya Haki za Binadamu ya Kikanda na Kimataifa, hivyo walemavu wanastahiliheshima ya utu wao kama Binadamu wengine kwa hiyo kitendo cha kuwapiga kuwaburuza na kuwadhalilisha na kuwaharibia nyenzo zao zinazowasaidia katika shughuli zao ni matumizi mabaya ya nguvu pamoja na mamlaka dhidi ya kundi hilo ’alisema Henga.

Kwa hiyo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC Tunalaani kwa nguvu zote kitendo kilichofanywa na jeshi la polisi dhidi ya kundi hili  kinyume na kifungu cha (4) cha Sheria ya watu wenye ulemavuya (2010) kanuni za msingi juu ya watu wenye ulemavu na Haki zao.

Akihitimisha tamko la Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Henga alisema kuwa jeshi la Polisi limefanya jambo ambalo linalokiuka kanuni na Sheria za nchi na kulitaka jeshi hilo lifanye kazi zake kwa mujibu wa Sheria ili kulinda raia na mali zake kama yalivyo makusudi ya kuanzishwa kwake.

‘Ifahamike kwamba watu wenye ulemavu kwa muktadha huohuo wamewekewa kinga dhidi ya mateso kwa nafasi yao kama kundi maalumu na pia kama kundi la binadamu wengine’alisema Henga.

Kwa upande wake   Mkurugenzi Mtendaji wa  Taasisi ya Haki za Binadamu na Maendeleo ya Kiuchumi kwa watu wenye ulemavu Daud Nyendo alisema kuwa jeshi la polisi lijitathmini upya juu ya matumizi ya nguvu hasa kwa watu ambao hawakuwa na silaha tena wakiwa ni kundi maalumu la walemavu kwa kuwaharibia mali zao na kuwafedhehesha na kulitaka jeshi hilo liache matumizi ya nguvu iliyopitiliza na kuwaomba Jeshi la polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam wajitokeze hadharani kuomba radhi  kwa walemavu hao kwa namna yoyote na Taifa kwa ujumla wake na kwamba lisipofanya hivyo litafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi.

Sanjari na hilo Mkurugenzi huyo amelitaka jeshi la Polisi litoe fidia kwa walemavu hao (waathirika) wa shambulizi hilo ambapo inakadiriwa kuwepo kwa uharibifu mkubwa wa mali zao ikiwemo baiskeli za walemavu hao (30) simu mbili ambazo hata hivyo thamani yake haikufahamika mara moja.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.