Ads Top

AGIZO LA JPM LASIMAMISHA SHUGHULI ZA KIJAMII KWA SAA MBILI




Na Antony Sollo Sumbawanga.

AGIZO la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli la kufanya siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi kuwa siku ya usafi wa mazingira le oleo limeleta simanzi na majionzi kwa wananchi wa Manispaa ya Sumbawanga na vitongoji vyake Tanzania Daima linaweza kuripoti.


Wakizungumza na Tanzania Daima wananchi waliokuwa wamekaa makundi katika mitaa mbalimbali wakisubiri tamko la Mkurugenzi wa Manispa ya Sumbawanga ili wafungue biashara zao wananchi hao wamelaani kitendo cha Ofisi ya Mkurugenzi kuwapa adhabu ya kufungua kinyume na tamko la Rais Magufuli ilivyozoeleka kwao ambapo kwa kawaida wamekuwa wakifungua saa nne baada ya kumaliza shuguli za usafi wa mazingira.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Zelothe Steven akiongozana na viongozi mbalimbali wa Manispaa ya Sumbawanga alipita katika maeneo mbalimbali kukagua zoezi la usafi wa mazingira ambapo msara huo ulianzia soko kuu na kuhitimisha katika soko la sabasaba.

Akiwa katika soko la sabasaba Mkuu huyo wa Mkoa alisikitishwa na hali ya soko hilo lilivyokuwa chafu na kuamuru viongozi wa Manispaa hiyo kusimamia vizuri majukumu yao na kuwataka watimize wajibu wao.

“ Nawaombeni kila mmoja atomize wajibu wake maana tukiwa tunasubiri siku iliyotamkwa na mh Rais tutakuwa hatujui vizuri wajibu wetu hivyo basi naomba kuwaambia ukweli kuanzia sasa mtumishi yeyote atakayezembea kutimiza wajibu wake hatutamvumilia”.alisema Zelothe.

Baada ya kukamilika kwa shughuli za usafi katika soko la sabasaba,Mkuu wa Mkoa aliwataka wananchi kuzingatia usafi ili kuzilinda Afya za wananchi.

“Ndugu zangu wananchi,naomba muelewe kuwa usafi siyo jambo la kupuuzwa maana Afya zetu ni muhimu kuliko kitu chochote hivyo jengeni tabia ya kufanya usafi bila kushurutishwa”alisema.

Kuhusu kucheleweshwa kufungua biashara kwa zaidi ya saa mbili wananchi wameilalamikia Serikali kutokana na uharibifu ambao umetokea kufuatia kuharibika kwa bidhaa zao zikiwemo nyanya,supu na samaki wabichi na kuiomba Serikali kuondoa mkanganyiko wa maelekezo ambapo kulikuwa na madai kuwa Mkurugenzi wa Manispa hiyo alitoa kauli tata kuwa wafanyabiashara wasifungue biashara zao mpaka hapo yeye atakapopenda jambo lililopingwa vikali na wananchi hao.

Mmoja wa wananchi hao Yusuf Masunga ameulalamikia uongozi wa Manispaa ya Sumbawanga kwa kushindwa kuheshimu sheria na kuziomba mamlaka zinazohusika kuwathamini wafanyabiashara maana ndiyo chanzo cha mapato ya Halmashauri ya Manispaa hiyo.

“Sisi wafanyabiashara ni wadau muhimu wa maendeleo ya Manispaa ya Sumbawanga,tunalipa ushuru,kodi, na mambo mengine sasa kitendo cha kutuzuia kufungua biashara zetu ni kukiuka maadili na haki maana iwapo tabia hii haitakemewa itafika mahala mtu mmoja atafikia uamzi wa kuamuru wananchi wakalale na wataamka atakapopenda yeye”alisema Mayunga.
                                
Tanzania Daima lilimtafuta Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Hamid Njovu ili kujibu tuhuma zilizotolewa kuhusu kauli ya kutofunguliwa kwa biashara mpaka yeye atakapopenda ambapo Mkurugenzi huyo aliruka futi miamoja kwa kuelekeza swali hilo aulizwe Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Zelothe Steven ambapo hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwamba hatuwezi kufanya shughuli za biashara bila kuzingatia usafi wa mazingira.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.