Ads Top

DIWANI ATOA AHADI HEWA UJENZI WA ZAHANATI

DIWANI wa Kata ya Ludete Sebastian Milando ( CCM ) anadaiwa kuwadanganya wapiga kura wake baada ya kuahidi kuchangia mifuko 25 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Mtaa wa Afya iliyoko katika Mtaa wa Afya Mji mdogo wa Katoro Mkoani Geita Tanzania Daima limeelezwa.

Wakizungumza na waandishi wa Habari wananchi wakazi wa Mtaa wa Afya wameeleza kusikitishwa na vitendo vya mwakilishi wao huyo ambaye ameshindwa kutimiza ahadi hiyo tangu alipoahidi septemba mwaka jana kwenye mkutano wa hadhara na kwamba diwani huyo alitoa kali ya mwaka Agosti mwaka huu baada ya kuibuka na kufanya ujenzi wa choo cha futi tatu katika Zahanati ya Mtaa wa Afya bila kumshirikisha Mwenyekiti wa Mtaa.

Wakati hayo yakifanyika Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Afya  Masaga Misso alikuwa anashikiliwa katika gereza la Biharamulo baada ya Viongozi 51 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kukamatwa wakiwa katika vikao vya Chama Wilayani Chato ambapo Viongozi hao walishikiliwa gerezani hapo kwa siku arobaini na tano

Mwenyekiti huyo wa Umoja wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Geita Masaga Misso alikamatwa akiwa na viongozi wenzake wa CHADEMA Mkoa wa Geita akiwemo Mwnyekiti wa Chama hicho Mkoa Fabian Mahenge, Mwenyekiti wa Balaza la Wazee Mkoa Vitus Makoye,Mwenyekiti,BAVICHA Neema Chozaile pamoja na

Hata hivyo baada ya Mwenyekiti huyo kutoka mahabusu ya Magereza Wilayani Chato alikutana na taarifa za kufanyika kwa ujenzi wa choo ambacho kinadaiwa kuwa na kina cha futi tatu na kwamba Misso alipiga marufuku mwendelezo wa ujenzi huo na kuamua kujenga choo cha kisasa kwa ajili ya kuhakikisha wakina mama katika Mtaa wake wanapata huduma nzuri.

“Mimi nawapenda wananchi wangu,siwezi kufanya ujenzi wa aina hiyo ni bora Diwani angeacha kufanya siasa katika masuala ya Afya za wananchi choo cha futi tatu! hivi akina mama wakitumbukia humo ni hasara ya nani?
Sasa mimi kama kiongozi niliyepewa dhamana ya kuongoza Mtaa huu nimeamua kujenga choo cha kisasa kitakachogharimu jumla ya shilingi 1,800,000.”alisema Misso.

Imeelezwa kuwa baada ya kukamatwa kwa Mwenyekiti huyo na kushikiliwa kwa siku arobaini na tano,Diwani huyo alitangaza kuwa Mwenyekiti huyo amefungwa na hatatoka gerezani hivyo alianza kampeni ya kupanga safu kwa ajili ya kufanyika kwa uchaguzi marudio na chanzo cha ujenzi wa choo hicho feki.

Mwenyekiti  huyo wa Serikali ya Mtaa wa Afya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Geita Masaga Misso, ameanza ujenzi wa choo cha kisasa pamoja na kukarabati majengo mawili ya Zahanati hiyo ambapo  ujenzi huo unatarajia kukamilika mapema septemba mwaka huu na kwamba ujenzi wa Choo hicho utagharimu kiasi cha shilingi mil 1,800,000 huku ukarabati wa majengo ya Zahanati ukigharimu kiasi cha shilingi mil 36 .

Tanzania Daima lilimtafuta Diwani wa kata ya Ludete  Sebastian Milando kuzungumzia tuhuma na malalamiko hayo ambapo alikana na kusema yeye hajui jambo lolote kati ya hayo yanayozungumzwa dhidi yake

“Mimi sijui chochote wacha waseme”alijibu  Milando na kukata simu.
MWISHO

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.