Ads Top

RAILA ODINGA AMEAPA KUENDELEA KUFANYA MAANDAMANO DHIDI YA UCHAGUZI WA UHURU KENYATTA AKISISITIZA KUWA UPINZANI HAUMTAMBUI


Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Nasa Raila Odinga
Odinga anasema kuwa Nasa haitambui uchaguzi huo kwa kuwa mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati pamoja na kamishna aliyejiuzulu Roselyn Akombe walithibitisha kwa umma kuwa tume hiyo haiwezi kusimamia uchaguzi ulio huru kutokana na misimamo ya kimapendeleo ya baadhi ya makamishna katika tume hiyo.
Odinga ambaye alikuwa akitoa mwelekeo wa upinzani kwa vyombo vya habari katika jumba la OKoa Kenya jijini Nairobi amesema kuwa ana ushahidi wa kutosha kwamba kulikuwa na uingiliaji na uongezaji wa kura katika ngome za chama tawala cha Jubilee.
Anasema kwamba iwapo uchaguzi huo utaruhusiwa na kutambulika utawavunja moyo Wakenya wengi na hivyobasi kuwafanya kutoshiriki katika uchaguzi mwengine wowote.
Mr Odinga pia amesema kuwa hawezi kuwaruhusu watu wawili wanaojigamba kuwa na uwezo kuharibu uhuru na demokrasia ilipatikana.
Amesema kuwa iwapo uchaguzi wa Uhuru utaruhusiwa kuna uwezekano kwamba ataingilia katiba na kuongeza muhula wa kuongoza.
''Tutaendelea kufanya maandamno kila mara'', alisema Raila Odinga.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.