Ads Top

WAZIRI MPINA ATOA SIKU MBILI NG’OMBE 640 ZIREJESHWE KWA WAFUGAJI




Waziri wa Mifugo na Uvuvi  Luhaga Mpina  akiwa  katika  pori la akiba  la Rukwa   Rukwati akiangalia baadhi ya ng’ombe  waliokufa wakiwa  wanashikiliwa na Taasisi ya Rukwa  Rukwati  ambapo jumla ya  mifugo hiyo 692  1mekufa kati ya mifugo 1332 iliyokuwa inashikiliwa .
Picha na  Mpiga picha Wetu

Na Antony Sollo -  Katavi
October 7, 2017
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina  ameupa siku mbili Uongozi wa Hifadhi ya Pori la Akiba la Rukwa – Lukwati kurejesha  mara moja  ng’ombe wapatao 640 waliosalia ambao ni mali ya wafujaji watatu kwa kuwa walikuwa wanashikiliwa  kwa muda wa mwaka mmoja kinyume cha Sheria.

Waziri Mpina alitoa agizo hilo  Oktoba 5 mwaka huu wakati alipotembelea hifadhi hiyo iliyopo katika Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Mlele  Mkoa wa Katavi  kwa lengo la kutatua mgogoro wa muda mrefu baina ya wafugaji hao watatu na uongozi wa hifadhi hiyo.

Imeelezwa kuwa ng’ombe wapatao  692 ambao  ni miongoni  1,332 walioshikiliwa na kuzuiliwa  katika Hifadhi ya Pori la Akiba la Rukwa – Lukwati  kwa zaidi  ya mwaka mmoja wamekufa kwa kukosa matunzo bora. 

Kufuatia hali hiyo Waziri Mpina alionyesha kushutushwa na taarifa iliyosomwa kwake na Meneja wa Hifadhi hiyo,Paschal Mhina  kuwa ng’ombe wapatao 1,332 waliovamia hifadhi walikamatwa  na kushikiliwa  kwa  mwaka mmoja na miezi tisa ambapo ng’ombe wapatao 692 wameshakufa  na waliobakia ni 640 tu .

Mpina aliuagiza uongozi  wa Serikali ya mkoa wa Katavi kuhakikisha  unahakiki mifugo hiyo na kuwakabidhi wenye mali na kwamba wale wote watakaobainika kusababisha  vifo vya ng’ombe hao waliokufa kwa uzembe wachukuliwe hatua kali za kinidhamu na za kijinai . 

“ Hakukuwa na sababu yoyote  ile ya  msingi ya kuendelea  kuishilikia  mifugo hiyo baada ya  wenye mali hiyo kufungua  mashitaka  mahakamani  ambapo  katika kesi ya awali watuhumiwa watatu ambao ndiyo wenye mali hiyo  walifungua mashataka  katika Mahakama ya  Wilaya ya  Mpanda   ambapo  mahakama hiyo iliamuru  itaifishwe na  iwe  mali ya  Serikali” alieleza  .

Waziri huyo alimtaka  Meneja wa  pori la  Akiba  amwonyeshe  hati yoyote  inayowapa   mamlaka ya  kuendelea kuwashikilia ngombe hao wakati  wafugaji  walikuwa  wanatuhumiwa  walikata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga  kupinga  kutaifishiwa  ngombe zao  lakini hakuweza kufanya hivyo.
Hata hivyo  imebainika kuwa  Mahakama Kuu  Kanda ya Sumbawanga ilitengua  hukumu iliyotolewa na  Mahama ya  Wilaya ya Mpanda na kuamuru  wafugaji hao watatu warejeshewe  mifugo yao  na faini ya Sh  500,000/- walizotozwa .
Wafugaji hao watatu  ni pamoja na Shigela Mayunga , Charles Mtokambali na Keleja Makuja .

 “Nimesikitishwa  sana na  kitendo cha  Uongozi wa hifadhi ya Pori la akiba la Rukwa  Lukwati kwa kuendelea kuishikilia mifugo hiyo ambapo idadi kubwa ya  mifugo hiyo imekufa kwa magonjwa nataka  kujua  kwa nini mifugo hiyo iliendelea kushikiliwa  ndani ya hifadhi hiyo  huku eneo hilo likiwa limetengwa maalumu  kwa ajili ya wanyamapori  na sio ng’ombe” alihoji  Mpina huku akionyesha hisia kali kufuatia ukatili uliofanywa.

Kwa upande wake  Meneja wa  Pori la  Akiba  la  Rukwa   Rukwati   Mhina  alieleza  kuwa mifugo hiyo ilendelea  kushikiliwa  kwa  kile alichodai  kuwa   baada  ya uongozi wa hifadhi hiyo kukata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa  na Mahakama  Kuu  Kanda ya Sumbawanga.

Akijitetea Mhina alisema kuwa ungozi wa hifadhi hiyo ulipewa maelekezo  na Mwanasheria Mkuu wa Serikali  kuwa waendelee kuitunza mifugo hiyo  kama sehemu ya kielelezo cha kesi hiyo .

Kwa upande wake ,  Katibu  Mkuu  wa  Chama cha Wafugaji  Tanzania Makoye Nkonosinema alisema kuwa mifugo  iliyokufa  ikiwa mikononi mwa uongozi wa hifadhi hiyo  wataendelea  kuidai.

Aidha alitaka kupewa maelezo ya kina  katika kipindi hicho chote ambacho ng’ombe hao walikuwa wameshikiliwa  ni ndama  wangapi waliozaliwa .

Naye  Ofisa Utafiti wa  Magonjwa ya  Mifugo wa  Mikoa wa Katavi  na Rukwa , Protus Reshola alisema kuwa idadi hiyo ya ng’ombe iliyokufa ni kubwa sana kwamba  imesababishwa na dosari kadhaa  ikiwemo waliokuwa wakiwachunga walikuwa sio wafugaji .

Aliongeza kuwa kutopatiwa matibabu stahiki na kutokuwepo na josho kwenye hifadhi hiyo  kumesababisha ng’ombe hao  kufa kutokana na ugonjwa wa homa ya mapafu .
Mwisho

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.