Ads Top

NI KUHUSU NG’OMBE 640 KUREJESHWA KWA WAFUGAJI

Na Antony Sollo -  Katavi
14 Nov, 2017.

UONGOZI wa Hifadhi ya Pori la Akiba la Rukwa – Lukwati unadaiwa kupuuza agizo lililotolewa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina  kuhusu kurejesha mara moja  ng’ombe wapatao 640 waliosalia baada ya Wafugaji waliokamatiwa Mifugo hiyo kulalamika kwa Waziri Mpina wakati wa Ziara yake katika Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Mlele  Mkoa wa Katavi  kwa lengo la kutatua mgogoro wa muda mrefu baina ya wafugaji hao watatu na uongozi wa hifadhi hiyo.

Mpina alitoa agizo hilo Oktoba 5 mwaka huu
baada ya kubaini kuwa Uongozi wa Hifadhi hiyo ulikuwa ukishikilia mifugo hiyo kinyume na Sheria kwa muda wa mwaka mmoja.

Ilielezwa kuwa,ng’ombe wapatao  692 ambao  ni miongoni 1,332 walioshikiliwa na kuzuiliwa  katika Hifadhi ya Pori la Akiba la Rukwa – Lukwati kwa zaidi  ya mwaka mmoja na kwamba walikufa kwa kukosa matunzo bora.

Kufuatia hali hiyo Waziri Mpina alionyesha kushutushwa na taarifa iliyosomwa kwake na Meneja wa Hifadhi hiyo,Paschal Mhina  kuwa ng’ombe wapatao 1,332 waliovamia hifadhi walikamatwa  na kushikiliwa  kwa  mwaka mmoja na miezi tisa ambapo ng’ombe wapatao 692 wameshakufa  na waliobakia ni 640 tu.

 Mpina aliuagiza uongozi  wa Serikali ya mkoa wa Katavi kuhakikisha  unahakiki mifugo hiyo na kuwakabidhi wenye mali na kwamba wale wote watakaobainika kusababisha  vifo vya ng’ombe hao waliokufa kwa uzembe wachukuliwe hatua kali za kinidhamu na za kijinai.

“ Hakukuwa na sababu yoyote  ile ya  msingi ya kuendelea  kuishilikia  mifugo hiyo hasa baada ya  wenye mali kufunguliwa Mashitaka katika Mahakama ya wilaya ya Mpanda ambapo  mahakama hiyo iliamuru  washitakiwa walipe faini ya shilingi laki tano na mifugo yao itaifishwa na iwe mali ya  Serikali ambapo wafugaji hao walikata Rufaa katika Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga na na Mahakama hiyo kutengua uamuzi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda” alisema Mpina.

Kufuatiahali hiyo,Waziri Mpina alimtaka  Meneja wa  pori la  Akiba  amwonyeshe  hati yoyote  inayowapa   mamlaka ya  kuendelea kuwashikilia ngombe hao wakati  wafugaji  walikuwa  wanatuhumiwa  walikata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga  kupinga  kutaifishiwa  ngombe zao  lakini hakuweza kufanya hivyo.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebainika kuwa  Mahakama Kuu  Kanda ya Sumbawanga ilitengua  hukumu iliyotolewa na  Mahama ya  Wilaya ya Mpanda na kuamuru  wafugaji hao watatu Shigela Mayunga , Charles Mtokambali na Keleja Makuja warejeshewe  mifugo yao  pamoja na faini ya Sh  500,000/- walizotozwa .

“Nimesikitishwa  sana na  kitendo cha  Uongozi wa hifadhi ya Pori la akiba la Rukwa – Lukwati kwa kuendelea kuishikilia mifugo hiyo ambapo idadi kubwa ya  mifugo hiyo imekufa kwa magonjwa nataka  kujua  kwa nini mifugo hiyo iliendelea kushikiliwa  ndani ya hifadhi hiyo  huku eneo hilo likiwa limetengwa maalumu  kwa ajili ya wanyamapori  na sio ng’ombe” alihoji  Mpina huku akionyesha hisia kali kufuatia ukatili uliofanywa.

Kwa upande wake  Meneja wa  Pori la  Akiba  la  Rukwa   Rukwati   Mhina  alieleza  kuwa mifugo hiyo ilendelea  kushikiliwa  kwa  kile alichodai  kuwa   baada  ya uongozi wa hifadhi hiyo kukata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa  na Mahakama  Kuu  Kanda ya Sumbawanga.

Akijitetea Mhina alisema kuwa ungozi wa hifadhi hiyo ulipewa maelekezo  na Mwanasheria Mkuu wa Serikali  kuwa waendelee kuitunza mifugo hiyo  kama sehemu ya kielelezo cha kesi hiyo ..

Akizungumzia kuchelewa kutekelezwa kwa agizo la Waziri wa Mifugo Katibu  Mkuu  wa  Chama cha Wafugaji  Tanzania Makoye Nkonosinema alisema ni kutokana na Mifugo hiyo kuonekana imeambukizwa Magonjwa baada ya kukosa huduma kwa kipindi kirefu hivyo shughuli inayoendelea hapo ni mifugo hiyo kutibiwa na madaktari wabobevu ambapo baada ya shughuli hiyo kukamilika Mifugo hiyo itarejeshwa kwa wafugaji kama Waziri alivyoagiza.

“Baaada ya uchunguzi wa kina kufanyika, imeonekana kuwa Mifugo hiyo imeambukizwa Magonjwa na ilikuwa na hali mbaya sana kiafya baada ya kukosa huduma kwa kipindi kirefu hivyo shughuli inayoendelea hapo ni mifugo hiyo kutibiwa na madaktari wabobevu kutoka Wizara ya Mifugo ambapo baada ya shughuli hiyo kukamilika Mifugo hiyo itarejeshwa kwa wafugaji chini ya usimamizi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda kama Waziri alivyoagiza”alisema Mkoye.

Kwa mujibu wa Makoye mifungo mingi iliyokuwa inashikiliwa hapo imekufa na kwamba Chama hicho kitahakikisha Serikali inarejesha Mifugo hiyo ikiwa ni pamoja na ongezeko la ng’ombe wanaodaiwa kuzaliwa lakini idadi inaonekana kubaki kama zilizvyokamatwa Magembe amemtaka Mkuu huyo wa Wilaya kutekeleza jukumu alilopewa na Waziri Mpina mapema.

Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Rachel Kasanda alipotakiwa kuzungumzia kucheleweshwa kwa utekelezaji wa agizo la waziri mpina alijibu kwa lugha kali,si uje ofisini? “mimi nina kikao halafu unaanzaje kuniuliza  kutotekelezeka kwa agizo la waziri? ni agizo lipi? agizo la waziri yupi! na lini? na umejuaje kama waziri amenipa maagizo? mpigie dc mpanda ndiye aliyetangaza kwenye TV”alisema kasanda na kukata simu.

Kutokana na hali hii inaendelea kuonyesha jisnsi baadhi ya wateule  Rais Magufuli wanavyoendelea na kupingana na Sera ya Uhuru na upatikanaji wa Habari kwa wananchi kupitia vyombo vya Habari kwa kutokuwa tayari kutoa ushirikiano kwa Waandishi wa Habari pindi wanapotakiwa kufanya hivyo,ambapo hadi sasa viongzozi hawa wameendelea kutupiana mpira juu ya nani anatakiwa kutekeleza agizo la Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Luhaga Mpina.

MWISHO.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.