Ads Top

WASHIKILIWA KWA KUPATIKANA NA BANGI.

Na Antony Sollo Mwanza.
Watu wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza kwa kosa la kupatikana na madawa ya kulevya aina ya bangi yenye uzito wa gramu 104.4.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Dcp: Ahmed Msangi ilisema kuwa tarehe 12.02.2018 majira ya saa 20:58 hrs usiku katika mtaa wa kiloleli kata nyasaka Wilaya ya Ilemela Mkoa wa Mwanza, askari wa jeshi la Polisi wakiwa  doria walipokea taarifa toka kwa raia wema kwamba katika mtaa wa Kiloleli kulikuwa na watu waliokuwa wanajihusisha na uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya aina ya bangi.

Baada ya  kupokea taarifa hizo Jeshi la Polisi walifanya upelelezi na msako katika maeneo hayo nakufanikiwa kuwakamata watuhumiwa shafii abdallah, (21), mkazi wa Mtaa wa Nyamanoro na John John,(19), mkazi wa Mtaa wa Kitangiri, ambao wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kupatikana na bangi kiasi cha gramu 104.4, kitendo ambacho ni kosa la jinai.

Taarifa ya Kamanda imeeleza kuwa Shafii abdalah alikutwa akiwa na bangi yenye uzito wa gramu 38 naJohn John akiwa na bangi kiasi cha gramu 66.4. ambapo Jeshi la polisi lipo katika mahojiano na watuhumiwa wote wawili pindi uchunguzi utakapokamilika watuhumiwa watafikishwa Mahakamani.

Aidha msako wa kuwatafuta watu wengine wanaoshirikiana kwa namna moja au nyingine na watuhumiwa wa biashara hiyo haramu ya madawa ya kulevya aina ya bangi bado unaendelea.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishina wa Polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa wakazi wa Jiji la Mwanza hususani vijana kuacha tabia ya kujihusisha na biashara haramu ya  dawa za kulevya kwani ni kosa kisheria.
Aidha anawaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu mapema ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

MWISHO.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.