Ads Top

AVUNJWA MKONO NA MWANAJESHI

Msichana aliyejitambulisha kwa jina la Pendo Benedict, 23, mkazi wa Goba wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam anadai kuvunjwa mkono na askari mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kile kilichoelezwa kuwa ni baada ya kumnyima penzi.
Pendo aliyefika katika ofisi za gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita, amedai kuwa askari huyo alimvunja mkono kwa kutumia mti baada ya kumpiga ambapo alimjeruhi sehemu mbalimbali za mwili Aprili 4, mwaka huu.

“Alinikuta katika banda la kuuzia chakula la mama ntilie ninakofanyia kazi, ni karibu na nyumba…

Pendo aliyefika katika ofisi za gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita, amedai kuwa askari huyo alimvunja mkono kwa kutumia mti baada ya kumpiga ambapo alimjeruhi sehemu mbalimbali za mwili Aprili 4, mwaka huu.

“Alinikuta katika banda la kuuzia chakula la mama ntilie ninakofanyia kazi, ni karibu na nyumba ya mwanajeshi huyo,” alidai Pendo.

Aliendela kusema kwamba siku hiyo ya tukio alimkuta akiendelea na kazi zake, ilipofika saa 3 usiku askari huyo alifika sehemu yake ya biashara na kumkuta akifanya mahesabu ndipo alipoanza kumtongoza, alipokataa alianza kumpiga.
“Nilipiga kelele na wananchi wakaja kuniokoa, nikajikongoja hadi nyumbani lakini cha kusikitisha bosi wangu hakunipa pole kutokana na majeraha niliyoyapata.
“Baada ya kujeruhiwa, Aprili 14, mwaka nilienda kutoa taarifa Kituo cha Polisi Kawe na kufungua kesi yenye jalada namba /RB/4227/2012, ambapo mtuhumiwa ambaye hivi sasa yupo huru alikamatwa na kuswekwa lupango.
“Hiyo haikuwa mara yangu ya kwanza kufanyiwa vituko na manyanyaso na mwanajeshi huyo na nilikuwa namueleza bosi wangu lakini hakujali, nikagundua kuwa alikuwa akila njama na askari huyo ili anipate kimapenzi.
“Kwa sasa bosi wangu hataki nikae naye, ninamshukuru Anati Murushi na mumewe ambao wamenipa hifadhi na kugharamia matibabu yangu.
“Polisi nimeandikisha kwamba mwanajeshi huyo amekuwa akinisumbua sana. Kuna siku nilitoka kuuza chakula saa 5 usiku, nilipoingia katika chumba nilichokua nalala nilimkuta askari huyo, nilimweleza bosi wangu lakini hakuchukua hatua zozote badala yake mwanajeshi huyo akaniambia nitakiona cha mtema kuni.
“Nilitoka kijijini kwetu Katoma Wilaya ya Bukoba Mach 11, mwaka huu kuja kufanya kazi ya kuuza chakula,” alisema Pendo.
Bosi wake aliyejitambulisha kwa jina la Bedastina Edward alipoulizwa alisema kwamba madai hayo siyo ya kweli bali amevunjwa mkono na mwanajeshi huyo baada ya kusikia kwamba ana mwanaume mwingine.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, alisema halijamfikia na kuahidi kulifuatilia.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.