Ads Top

WAKUTWA WAKIFUKUA KABULI

                                                         KABURI LILOFUKULIWA

                                           WILLIAM JOEL ENZI ZA UHAI WAKE
Na Juma hasani Nyete
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, maiti ya William Joel Shechambo,74 , aliyefariki dunia Novemba 19, 2011 na kuzikwa Novemba 23, 2011 katika Kijiji cha Maivaro mkoani Arusha imefukuliwa, hivyo polisi kutupiwa lawama.
Tukio hilo la aina yake la kufukuliwa kwa kaburi la maiti hiyo, lilifanyika usiku wa kuamkia Desemba 8, mwaka jana ambapo waliofanya kitendo hicho walifumwa na ndugu wa marehemu lakini licha ya kuripoti polisi, hakuna aliyekamatwa.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, mtoto wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Meja Renatus Masunde alisema kuwa eneo hilo ni mali ya wazazi wake ambao wametangulia mbele za haki na wamelimiliki kwa zaidi ya miaka 50.
“Mama yangu Sesilia Masawe alikuwa na kaka yake aitwaye Francis Masawe, alimpa eneo hili mwaka 1960, tumeshazika zaidi ya ndugu watatu, hawakuja kufukua maiti zao,” alisema Masunde.
Aidha, Masunde alidai kwamba vurugu za kugombea eneo hilo zilianzishwa na ndugu wa upande wa mama yake ambao walidai ni mali yao.
Kamanda huyo wa jeshi alidai kuwa kufukua maiti ni kosa la jinai, hivyo walikwenda kuripoti Kituo cha Polisi Kati Arusha kwa kuwa watuhumiwa wanafahamika ambapo walifunguliwa jalada na AR/RB/15455/2011.
Alisema polisi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja lakini baada ya siku chache aliachiwa bila kuambiwa sababu hali iliyomfanya amuone Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai nchini, Robert Manumba ambaye alimrudisha kwa Afisa Upelelezi wa Mkoa (RCO).
Hata hivyo, RCO alimkabidhi kwa mkuu wa polisi wa wilaya ambaye hakushughulikia chochote hali inayofanya familia ya marehemu ijiulize kwa nini watuhumiwa hawakamatwi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye alipoulizwa juu ya tukio hilo alisema halijamfikia na kuahidi kulifanyia kazi.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.