Ads Top

WAZIRI WA UCHUKUZI ATAKIWA KU JIUZULU

Wapiga mzigo (wafanyakazi) wa Shirika la reli la (TAZARA) wamemtaka Waziri wa Uchukuzi Bw, Omari Nundu ajiuzulu kutokana na kushindwa kusimamia madai yao ya mwezi januari na februari.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wenzake mmoja wa Wanyakazi wa Shirika hilo ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema kuwa,takwimu zinaonyesha shirika hilo linaingiza zaidi bilioni tatu kwa mwezi.

Alisema kutokana na kutokuwa na usimamizi mzuri wa pesa hizo kumepelekea wafanyakazi wa shirika hilo kutolipwa madai yao kwa muda muafaka.

Aliongeza kuwa Viongozi hao wakijiuzulu kutasidia kwa kiasi kikubwa Shirika hilo kuafanya kazi kwa uafanisi pamoja na kuondoa migogoro inayojitokeza katika shirika hilo.

``Takwimu zinaonyesha shirika linaingiza biloni tatu kwa mwezi,na sisi tunadai bilioni 1.1 za mshahara kwa wafanyakazi kwa nini tusilipwe pesa zetu kwa wa wakati muafaka kwasababu wengine tunategemewa na familia zetu ili kuendesha maisha yetu``alisema na kuongeza.

Hata hivyo aliongeza kuwa Viongozi wa Serikali wamekuwa na tabia za kupeleka taarifa za uwongo Wizarani kwakusema Shirika hilo halina matatizo yoyote.

``Kumemekuwa,, na tabia ya baadhi ya Viongozi kusema uwongo kwenye Shirika letu hakuna matatizo yoyote,lakini ukinaglia kwa namna au nyingine ndani ya shirika letu kuna matatizo mengi.

Alisema kuwa, hatua ya mwisho waliyoifikia ni Waziri wa Uchukuzi Bw Omari Nundu ajiuzulu kutokana na kushindwa kusimamia madai yao.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.