Ads Top

SHEIKH FARID APATIKANA

 Sheikh Farid, akipokewa na ndugu na jamaa nyumbani kwake
 Kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho visiwani Zanzibar, Sheikh Farid, (Wapili kushoto), akipiga picha ya ukumbusho na familia yake mara baada ya kjuwasili nyumbani kutoka kusikojulikana, Ijumaa Oktoba 19, 2012
Sheikh Farid, na baadhi ya wafuasi wake, wakiomba dua nyumbani kwake mara baada ya kupatikana, Ijumaa Oktoba 19, 2012-
--
Kuna habari kuwa kiongozi wa Jumuiyab ya Uamsho, kisiwani Unguja, Zanzibar, Sheikh Farid amepatikana nay u salama salimin.

Picha za mitandao zinaonhyesha sheikg huyo mwenye msimamo makali alionekana akilakiwa na watu b waliotajwa kuwa ni ndugu na jamaa, ambapo picha nyingine zinaonyesdha akiwa na familia yake na moja ikionyesha akiomba dua nyumbani kwake.
Kwa mjujibu wa taarifa za mkitandao, Sheikh huyo aliyetoweka tangu Oktoba 16, 2012 na kuonekana tena Oktoba 19, 2012 majira ya jioni, alisema, “alichukuliwa na watu waliojitambulisha kwake, kuwa ni askari polisi na baadhi yao wakiwa na silaha.”. Alisema

|Nilifungwa kitambaa cheusi usoni na kupelekwa nisikokujua” alifafanua sheikh huyo.

Amedai askari hao wenye lafudhi za Tanzania Bara na wengine Visiwani, walitaka kujua kuhusu harakati zake zikiwemo safari zake za nje zikiwemo za Uarabuni na mahusiano yake na baadhi ya viongozi wa serikali.

Pia askari hao walichukua simu yake na kumuhoji mengi kuhusu namba na message zilizopo kwenye simu yake. Watu hao walimrudisha eneo walilomchukua wakamfungua pingu na kitambaa cha usoni kisha wakamuachia huru.

Alisema watu hao waliomchukua kwa gari walikuwa wanne, akiwepo dereva na mwingine aliyekaa mbele ambaye alijitambulisha kwake, na nyuma ya gari walikuwepo watu wawili waliovaa kofia zilizofunika nyuso zao

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.