CLOUDS WAMPELEKA LADY JAYDEE MAHAKAMANI
Taarifa
zilizotufikia ambazo bado zipo chini ya kapeti ni kwamba Kampuni ya
Clouds Media Group, imeamua kumfungilia mashitaka msanii nguli wa Bongo
Fleva na kiongozi wa bendi ya Machozi, Judith Wambura Mbibo ‘Lady
Jaydee’. Clouds imeamua kufungua mashitaka hayo baada ya Lady Jaydee
kuchafua jina la kampuni hiyo na viongozi wake wawili wa juu ambao ni
Mkurugenzi Mtendaji, Joseph Kusaga na Mkurugenzi wa Utafiti na
Maendeleo, Ruge Mutahaba katika mitandao ya kijamii hivi karibuni. Lady
Jaydee anatakiwa kuripoti katika Mahakama ya Kinondoni kukabiliana na
tuhuma hizo hapo kesho.
No comments: