Dar es Salaam/Arusha. Utata wa kidiplomasia ulioibuka kuhusu raia wa kigeni kukamatwa wakituhumiwa kwa mlipuko wa bomu katika Kanisa Katoliki umemlazimu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kutua jijini Arusha kusawazisha mambo
Membe alisema jana kuwa atakwenda huko kufuatilia
suala hilo na hasa kwa kukamatwa raia wa kigeni wakihusishwa na tukio
hilo, wakiwa ni miongoni mwa watu 12 wanaoshikiliwa na polisi
wakituhumiwa kuhusika na shambulio hilo lililoua watu watatu na wengine
zaidi ya 60 kujeruhiwa.
“Ninakwenda Arusha kesho (leo) ili kufahamu undani
wa suala hili. Baada ya kwenda ndiyo nitakuwa katika nafasi ya
kuongelea mambo haya,” alisema Membe wakati alipoulizwa jana kuhusu
malalamiko ya nchi za Saudi Arabia na Falme za Kiarabu (UAE) kuhusu
kukamatwa kwa raia wao.
Watu wanaoshikiliwa na polisi kwa tuhuma hizi ni
pamoja nja Victor Ambrose Calist (20), Mwendasha Bodaboda na mkazi wa
Kwa Mrombo, Jeseph Yusuph Lomayani (18) mwendesha Bodaboda, Mkazi wa Kwa
Mrombo jijini Arusha.
Wegine ni George Batholomeo Silayo (23),
mfanyabiashara na mkazi wa Olasiti, Arusha, Mohamed Sulemani Said (38)
mkazi wa Ilala, Dar es Salaam na Jassini Mbaraka (29) mkazi wa Arusha.
Wale wanaotuhumiwa kutoka nje ya Tanzania ni
pamoja na raia wa Falme za Kiarabu (UAE), Said Abdalla Said (28),
Abdulaziz Mubarak (30) na Said Mohsen wakati Jassini Mbaraka (29)
anatokea Saudi Arabia
Hata hivyo, suala la kukamatwa kwa raia wa nchi za kigeni limezua utata wa kidiplomasia kutoka nchi za Saudi Arabia na UAE.
Gazeti dada la The East African limekariri vyanzo
vyake vikidai kuwa mabalozi wa nchi hizo wanataka kuandika barua ya
malalamiko kwa Serikali ya Tanzania kupinga kukamatwa kwa raia wao, pia
kutangazwa kwenye vyombo vya habari.
Mabalozi wa nchi hizo za Mashariki ya Kati
walifuatana na wanasheria wao kwenda kuangalia hali za watuhumiwa kutoka
nchi zao huko Arusha.
Balozi wa Saudi Arabia, Hani Abdalla Momenah
aliliambia gazeti la Al-Hayat la Saudi Arabia akidai mtu wake alikamatwa
kwa hisia tu na kwamba asingeondoka Arusha hadi kieleweke.
“Watu hawa wamekamatwa kwa hisia tu ila nina
uhakika wataachiwa kwa mapenzi ya Mungu. Walikuwa wamekuja kutalii
Tanzania,” aliongeza Momenah.
Wakati mtuhumiwa raia wa Tanzania Ambrose anayetuhumiwa kwa kumbeba kwenye pikipiki ndiye aliyehusika na ulipuaji.
Hatima kujulikana leo
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas aliliambia
Mwananchi jana kuwa taarifa kamili za watuhumiwa wa tukio hilo
zitatolewa leo kama waliokamatwa watafikishwa mahakamani au la.
“Kesho (leo) tutatoa taarifa zote, uchunguzi ulipofikia na watuhumiwa wote baada ya upelelezi,” alisema Kamanda Sabas.
Wasiwasi makanisani
No comments: