Wiki kadhaa zimepita tangu mwanamuziki mkongwe, Juma Kassim Nature atangazwe katika vyombo mbalimbali vya habari kuwa aliwahi kulewa na kuhudhuria mahojiano aliyotakiwa kufanyiwa katika kituo kimoja cha redio nchini.
Akizungumza na Mwananchi, Nature aliweka wazi kuwa
alikunywa pombe lakini hakulewa kama inavyodaiwa licha ya kwamba alivaa
ndala alivyokwenda katika mahojiano hayo.
“Ningependa mashabiki wangu wafahamu na kuelewa
kwamba lile tukio ambalo limenitokea katika kituo kimoja cha redio
katika mahojiano yale kwa madai kwamba nilikuwa nimevaa ndala, pia
nilikuwa tayari nimeshalewa si kweli,” alisema Nature.
Hata hivyo, msanii huyo alikiri wazi kuwa
alikunywa pombe lakini aliweza kujimudu hata kuendesha gari lake kutoka
nyumbani kwake hadi studio.
“Endapo mtu amekunywa pombe kisha akawa bado
anaufahamu wa kuweza kwenda mahali na kujielezea mpaka kuendesha gari,
huyo mtu hajalewa ila tunasema kwa lugha nyepesi amekunywa.
“Nafahamu kwamba msanii ni kioo cha jamii. Kila
msanii wa fani yoyote huwa anakuwa na staili yake ya kutoka au kwa hapa
nchini tunasema ‘nitoke vipi’, sasa mimi nashangaa leo wanasema Kiroboto
kavaa ndala wakati wamesahau kuna mastaa wakubwa tena wenye majina
duniani wanavaa vitu ambavyo huwezi hata ukaviongelea. Mfano mzuri ni
mwanadada Lady Gaga ingekuwa yule ndiyo yupo Bongo na akaenda kwenye
mahojiano na vazi la nyama kama lile alilovaa, wangemtoa?
Akimalizia Nature aliweka wazi kuwa ameshatangaza
kusitisha kupeleka kazi zake katika kituo hicho, pia kuwataka waache
kuzirusha hewani kazi zake.
No comments: