HIVI NDIVYO ILIVYO KUWA KATIKA SWARA ZIMA LAW KUAGA MWILI WA MWANAMUZIKI MASHUHURI NCHINI MAREHEMU ALBERT MANGWAIR JIJINI DAR ES SALAAM
Ilikuwa ni simanzi kwawale hasa
waliokuwa wakipata Burudani kutoka kwa Albert Mangwair na hakika
aliyethibitisha kwa kuona kuwa sasa amelala na hainuki hadi Masiha
atakapo rudi walishindwa kujizuia kwa vilio kama Rasta huyu kutoka
Ukonga Mazizini maarufu kwajina la Simaga akitokwa na machozi baada ya
kutoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Albert Mangwea katika
viwanja vya Lidaz Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mamia ya Wakazi wa jiji walijitokeza
kumuaga Msanii huyo wa muziki wa kizazi kipya aliyefariki Mei 28, mwaka
huu Nchini Afrika Kusini alikokuwa kwa shughuli za kimuziki.
Mangwewa alisafirishwa mchana wa leo kwenda Kihonda mkoani Morogoro kwa mazishi yatakayo fanyika kesho.
Huyu
naye ambaye haikuweza kufahamika jina lake kwa haraka, akipiga picha
huku akiangua kilio wakati wa kuaga mwili wa marehemu.....
Wanafamilia wakipita kuaga mwili wa ndugu yao....
Mbunge wa kinondoni Idd Azzan anamuaga Ngwea
P. Funky akipita kuaga na kutoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la Mangwea
Wasanii wa Bongo Movie wakipita kutoa heshima za mwisho kwa Mwili wa marehemu
Hata wanahabari nao kama Issa Mnali walitoa heshima za mwisho.
Rais wa
Shirikisho la Muziki Tanzania, Addo Novemba kushoto akijadiliana jambo
na viongozi wa Kamati ya Mazishi katika shughuli yaa kumuaga marehemu
Albert Mangwea, katika viwanja
vya Leaders Club leo.
Ras Simaga akipita na zana zake baada ya kutoa heshima za mwisho.
Miraji Kikwete akizungumza machache na Ummy Wenselaus 'Dokii' viwanja vya Lidaz
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kuaga mwili wa marehemu Mangwea
Sehemu ya
waombolezaji waliokwenda kumuaga marehemu Ngwea wakionekana katika viwanja vya Leaders Club leo.
Mwenyekiti
wa Baraza la Vijana la Taifa Chadema (BAVICHA), John Heche wa tatu
kutoka kushoto akijadiliana na viongozi wenzake waliokwenda kuaga mwili
wa marehemu Albert Mangwea leo viwanja
vya Leaders Club leo.
Wadau wakubwa wa kazi za Ngwair wakiwa katika pozi la majonzi.
Kamati ya Maandalizi ya Mazishi ya Ngwair ikiwa jukwaani.
Gari ya polisi ikiongoza msafara wa
magari mengine kuelekea mkoani moogoro muda mfupi baaada ya mamia ya
mashabiki na wananchi wa jiji la Dar es Salaam na Vitongoji vyake kutoa
heshima za Mwisho kwa mwili wa msaniii mashukuri nchini albert
Mangwea.Picha Na Mdau Mbwana Ramadhania
No comments: