MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa amekipa usajili wa kudumu Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA)
Gari la Mwenyekiti wa muda wa CHAUMMA, Wallance Mayunga likiondoka baada ya hafla ya usajili.
Tendwa akikabidhi cheti cha usajili CHAUMMA.
Wanachama wakionesha cheti cha usajili kwa wanahabari.
Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, John Tendwa (kulia) akizungumza na wana CHAUMMA.
Na Thehabari.com
MSAJILI wa
Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa amekipa usajili wa kudumu Chama cha
Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) huku akivitaka vyama vya siasa kufuata sheria na
kuepuka kuwa vyanzo vya vurugu na uchochezi wa migogoro.
Tendwa
ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwakabidhi cheti cha
usajili wa kudumu viongozi wa chama kimpya cha kinachojulikana kama Chama cha
Ukombozi wa Umma.
Alivitaka
vyama vya siasa kuhakikisha vinatimiza malengo yao ya kushika dola na hata kama
itashindikana kwao, basi kuhakikisha wanapata nafasi za uwakilishi wa wananchi
zikiwemo za udiwani, ubunge pamoja na uongozi wa serikali za mitaa kwa mujibu
wa taratibu za nafasi hizo.
Alisema kwa
sasa vipo vyama vya siasa ambavyo licha ya kuwa na usajili wa kudumu na uongozi
mzuri usio na migogoro vimeshindwa kutimiza malengo ya msingi ya chama kwa
kushika nafasi za uwakilishi maeneo anuai kwa mujibu wa utaratibu.
“…Vyama hivi
unakuta hawana mbunge, hawana diwani, hawana viongozi serikali za mitaa, kijiji
na kwingineko lakini ukiangalia wana viongozi wazuri hawana migogoro ndani ya
chama, haya sio madhumuni ya chama cha siasa,” alisema Tendwa.
Aidha
aliwataka viongozi wa CHAUMMA kuhakikisha wanajipanga vizuri ili waweze
kutimiza malengo ya chama na kuwawakilisha wananchi maeneo mbalimbali ya
uongozi kisiasa. Alisema katika mapendekezo mapya ofisi yake inafikiria kuanza
kuvipunguza vyama ambavyo licha ya kuwa na usajili havifanyi chochote kama
ilivyo kwa madhumuni ya kuanzisha chama.
“Sheria
inafanyiwa marekebisho, chama kikikaa ndani ya miaka mitano hakijafanya
chochote tunafikiria kukifuta, kiongozi wa chama akitukana miezi sita
unafungiwa kwa muda…maana hatuwezi kuruhusu matusi, vurungu na masuala mengine
yasiokuwa na msingi ndani ya vyama vya siasa,” alisema Tendwa.
Hata hivyo
amesema katika mapendekezo yao ya mabadiliko ya katiba wamependekeza mambo
mengi ikiwemo sasa kuruhusu vyama kujiunga na kufanya shughuli za siasa kama
ilivyo kwa nchi za Kenya, Afrika Kusini, Lethoto na nchini Namibia.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhiwa cheti cha usajili wa kudumu Mwenyekiti wa muda wa
CHAUMMA, Wallance Mayunga alisema wamejipanga vizuri katika kuwatumikia
wananchi na chama chake kinatambua changamoto zilizopo nchini katika uongozi,
utendaji na utawala hivyo kina nia ya kuleta mabadiliko.
Nafasi ya
Katibu Mkuu wa muda wa CHAUMMA inashikiliwa na Shaffii Abed huku Hamad Tao
akiwa ni miongoni mwa wanachama waanzilishi wa nchama hicho
No comments: