RAIS JAKAYA KIKWETE AWAANDALIA MARAIS DHIFA YA KITAIFA YA CHAKULA CHA USIKU
Rais
Jakaya Kikwete akizungumza na Mfalme wa Swaziland, King Mswati katika
hafla ya chakula cha usiku alichokiandaa kwenye viwanja vya Gymkhana,
Dar es Salaam jana usiku, kwa waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa
Ushirikiano wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa Manufaa ya Wote
(Global Smart Partinership Dialogue). TBL ni moja kati kampuni
zilizofadhli hafla hiyo.
Mahali palipoandaliwa kwa dina kwenye viwanja vya Gymkhana
Rais
wa zamani wa Msumbiji, Joachim Chisano (kushoto) akikaribishwa na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernald Membe katika
hafla ya chakula cha usiku.
JK akiwa na Museveni wa Uganda (kushoto), Kingi Mswati wa Swaziland na Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi
Mjumbe
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Alnold Kilewo
(kushoto), akiwa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Chibuku cha Dar Brew,
Kilowi Suma (wa pili kushoto), katika hafla ya chakula cha usiku
iliyoandaliwa na Rais Jakaya Kikwete kwa marais na viongozi mbalimbali
waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Maendeleo ya
Sayansi na Teknolojia kwa Manufaa ya Wote (Global Smart Partinership
Dialogue). Kutoka kulia ni Kiongozi wa mabalozi wanaoziwakilisha nchi
zao hapa nchini, Halfan Mpango na Mkurugenzi wa Mfuko wa Sekta Binafsi
Tanzania (TPSF), Esther Mkwizu. Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ni kati
ya kampuni zilizofadhili hafla ya chakula hicho.
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni akihutubia katika hafla hiyo.
Rais
Jakaya Kikwete akiwaongoza baadhi ya marais na viongozi wengine kucheza
muziki uliokuwa ukiporomoshwa na kikundi cha sanaa cha Tanzania House
of Talent (THT), wakati wa hafla ya chakula cha usiku
Rais
Jakaya Kikwete akiwaongoza baadhi ya marais na viongozi wengine kucheza
muziki uliokuwa ukiporomoshwa na kikundi cha sanaa cha Tanzania House
of Talent (THT), wakati wa hafla ya chakula cha usiku alichokiandaa
viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam jana usiku, kwa marais na viongozi
waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Maendeleo ya
Sayansi na Teknolojia kwa Manufa ya Wote (Global Smart Partinership
Dialogue). Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ilikuwa kati ya kampuni
zilizofadhili hafla ya chakula hicho.
Bendi ya THT ikitumbuiza katika hafla hiyo
Msanii
Mwasiti akipongezwa na Mbunge wa Afrika Mashariki, Adam Kimbisa. Kulia
ni Mbunge wa bunge hilo, Shy Rose Bhanji na Abdul Mwinyi ambaye pia ni
Mbunge wa Bunge hilo
Kimbisa akiwa na Mwinyi, Bhanji na Richard Kasesera
No comments: