MAISHA YA MZEE MADIBA
BABA wa Taifa la Afrika Kusini na kipenzi cha wengi, Nelson Rolihlahla Madiba Mandela ‘Mzee Madiba’ (94), anabaki kuwa mmoja wa mashujaa walioongoza vita dhidi ya ubaguzi wa mtu mweusi hapa duniani ukiwaacha akina Martin Luther King aliyekuwa uhamishoni Marekani, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania, Patrick Lumumba wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, zamani Zaire, Nkwame Nkuruma wa Ghana na wengineo.
Kwenye makala haya sitazungumza ‘profaili’ ya Mzee Madiba isipokuwa nimenyofoa kipengele kimoja tukijadili.
Tunajua katika maisha kuna wakati mtu unakutana na vipingamizi vya kufikia malengo kutoka ndani ya familia au jamii inayokuzunguka.
MCHANGO WA KIFAMILIA
Baba yake alifariki dunia wakati Mzee Madiba akiwa na umri wa miaka tisa tu kwa hiyo hakuna mchango wa mzazi huyo kwenye harakati zake.
Alipoanza mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi na kutafuta usawa kwa wote, ilitegemewa kuwa mkewe ndiye angekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mafanikio yanapatikana.
Tunajua katika maisha kuna wakati mtu unakutana na vipingamizi vya kufikia malengo kutoka ndani ya familia au jamii inayokuzunguka.
MCHANGO WA KIFAMILIA
Baba yake alifariki dunia wakati Mzee Madiba akiwa na umri wa miaka tisa tu kwa hiyo hakuna mchango wa mzazi huyo kwenye harakati zake.
Alipoanza mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi na kutafuta usawa kwa wote, ilitegemewa kuwa mkewe ndiye angekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mafanikio yanapatikana.
Mzee Madiba alioa mara tatu. Mke wa mwisho alimuoa alipokuwa akiadhimisha miaka 80 ya kuzaliwa.
Mzee Madiba katika kipindi chote cha historia ya maisha yake amekuwa mtetezi wa watoto kupitia Mfuko wa Nelson Mandela wa kusaidia watoto.
Mzee Madiba ni baba wa watoto sita. Wanne aliwazaa na mkewe wa kwanza, Evelyn Mase na wawili alizaa na mke wake wa pili, Winnie Madikizela Mandela.
Baadhi ya watoto wake hawakwenda kumuona wakati akiwa gerezani.
Maajabu! Watoto wake wote wawili wa kike aliowazaa na mke wa kwanza walikuwa wakitumia jina la Makazawie!
Mtoto wake wa kwanza alifariki dunia akiwa na umri wa miezi tisa na mtoto wa pili aliyejulikana kwa jina la Madiba Thembikile (Thembi) alifariki dunia katika ajali ya gari mwaka 1969 akiwa na umri wa miaka 25.
Masikini! Mzee Mdiba wakati huo alikuwa gerezani na hakuruhusiwa kwenda kuhudhuria mazishi ya mwanaye.
Mwanaye Makgatho alifariki dunia kwa Ugonjwa wa Ukimwi mwaka 2005. Watu walipotaka kuficha kilichomuua, Mzee Madiba aliingilia kati na kusema hadharani kuwa Ukimwi ndiyo umemuua! Kuanzia hapo Mzee Madiba amekuwa mstari wa mbele kupiga vita Virusi vya HIV na Ukimwi akitumia namba 46664 ambayo ni namba aliyopewa alipokuwa gerezani.
Mzee Madiba na Evelyn walidumu katika ndoa yao kwa miaka 13 kabla ya kuvunjika mwaka 1957.
Evelyn alikuwa muumini wa Dhehebu la Mashahidi wa Yehova ambalo lilikuwa haliruhusu waumini wake kushiriki kwenye siasa, akashindwa kumsapoti mumewe, Alifariki dunia mwaka 2004.
Mwaka mmoja baadaye,1958 Mzee Madiba alimuoa Winnie Madikizela. Winnie Madikizela Mandela aliyezaliwa Sauzi Septemba 26, 1936. Ni mwanasiasa aliyewahi kushika nafasi kadhaa serikalini, kama vile African National Congress Women’s League. Kwa sasa ni mwanachama katika Chama cha National Executive Committee. Japokuwa aliolewa na Mzee Madiba, wakati mzee huyo anapata urais hakuwa ‘first lady’ kwani wawili hao, waliachana miaka miwili baadaye kwa madai ya kuwa Winnie, alikuwa siyo mwaminifu baada ya Mzee Madiba kutoka gerezani ambapo alimpa talaka rasmi Machi 19,1996.
Pamoja na kuwa mpiganiaji haki na maarufu kwa wanachama wake ambao humwiita ‘Mama wa Taifa’ lakini alishindwa kuzuia tamaa ya mwili na kujikuta akimsaliti Mzee Madiba.
Muda mwingi hawakuishi pamoja kwa sababu Mzee Madiba alikuwa akitumikia kifungo huku Winnie akijijengea umaarufu katika majukwaa ya siasa.
Mwaka 1998, Mzee Madiba alimuoa Graca Machel ambaye alikuwa mke wa kwanza wa Rais wa Msumbiji, Hayati Samora Machel. Wameishi wote katika siku zao za uzeeni huku wakipeana sapoti ya hali ya juu bila mtoto.
No comments: