Takriban watu 37 wamekufa baada ya kugongwa na treni wakati wakivuka njia ya reli katika jimbo la Bihar, India
Maafisa wamesema wengi wa abiria walikua mahujaji wa Ki-Hindi waliokua
wametua katika kituo kimoja cha eneo la Dhamara Ghat na walikua njiani
kuelekea Hekalu iliyoko Wilaya ya Saharsa.
Ajali hiyo ilipelekea ghathabu ya raia ambao waliteketeza mabehewa ya
treni hiyo. Makundi ya wokozi yanaendelea kutafuta manusura na polisi
wa kuzima ghasia wametumwa eneo la ajali.
Mkuu wa pilisi katika jimbo la Bihar amesema
haijathibitishwa idadi kamili ya watu waliokufa, kwani vipande vipande
vya miili ya watu imetapakaa eneo hilo.
Maafisa wa huduma ya reli wamesema treni hiyo ya
mwendo wa kasi ilikikuwa njiani na haikutarajiwa kutua kituo cha
Dhamara Ghat. Hata hivyo ilisimama baada ya ajali kutokea ambapo umati
wa watu ulishambulia dereva na kumjeruhi vibaya.
Huduma ya treni inamilikiwa na serikali nchini
India na inawahudumia abiria milioni 18 kila siku.Serikali imesema zaidi
ya watu laki moja unusu waliuawa na treni mwaka jana pekee wakati
wakivuka njia ya reli inayotumika na treni za mwendo wa kasi.
Kwa habari zaidi bofya hapa......>>>>>>>>>
Kwa habari zaidi bofya hapa......>>>>>>>>>
No comments: