Takriban maafisa 24 wa polisi kutoka Misri wameuawa kwenye shambulizi la kuvizia katika eneo la Rasi la Sinai
Duru zinaarifu polisi hao walikuwa kwenye msafara wa mabasi mawili
yaliyoshambuliwa na kundi la watu waliokua na silaha karibu na mji wa
Rafa mpaka na Ukanda na Gaza.
Polisi watatu walijeruhiwa kwenye shambulio hilo. Katika siku za karibuni jeshi la Misri limeimarisha operesheni dhidi ya wanamgambo eneo la Sinai hususan baada ya mashambulizi kuongezeka tangu kuanguka kwa uliokua utawala wa Hosni Mubarak mwaka 2011.
Polisi watatu walijeruhiwa kwenye shambulio hilo. Katika siku za karibuni jeshi la Misri limeimarisha operesheni dhidi ya wanamgambo eneo la Sinai hususan baada ya mashambulizi kuongezeka tangu kuanguka kwa uliokua utawala wa Hosni Mubarak mwaka 2011.
Misri imekua ikishika doria eneo la
Sinai chini ya mkataba wa mwaka 1979 kati ya Israel na Misri.Mashirika
ya habari yanaripoti kwamba wanaume wanne waliojihami kwa silaha
walisimamisha mabasi hayo na kuwaamrisha abiria wote kuondoka kisha
wakaanza kuwapiga risasi.
Baadhi ya duru zinasema washambuliaji hao
walitumia maroketi kulenga mabasi hayo. Utawala wa mpito umetangaza hali
ya hatari kufuatia maandamano ya umma yaliofuatia kuondolewa mamlakani
kwa Muhammed Morsi kama Rais wa nchi hiyo. Amri ya kutotoka nje usiku
imewekwa mji mkuu Cairo.
Zaidi ya watu 800 wakiwemo polisi 70 wameuawa
tangu Jumatano ya wiki jana wakati jeshi lilipovunja kambi za wafuasi wa
vuguvugu la Muslim Brotherhood anakotokea Morsi. Na hapo Jumapili
mahabusu 36 walikufa wakati wakisafirishwa katika jela moja nje ya mji
wa Cairo.Serikali na jeshi wamesema mahabusu hao walikosa hewa kwenye
gari walimokua. Hata hivyo Muslim Brotherhood wametaja kitendo hicho
kama mauaji ya kinyama.
No comments: