Bibi mmoja raia wa Nigeria, Olabisi Ibidun Cole (65) amevunja rekodi ya umri wa watu wanaokamatwa wakiwa na dawa za kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA

“Huyu ni mzee, lakini tumeshangaa kuona bado ana nguvu za kutosha na
tulishangaa baada ya kutoa kete 20 kwa mara moja katika awamu ya kwanza,
jambo hili si rahisi kutokana na umri wake,”.
Bibi mmoja raia wa Nigeria, Olabisi Ibidun Cole (65) amevunja
rekodi ya umri wa watu wanaokamatwa wakiwa na dawa za kulevya katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Cole alikamatwa Jumatatu akiwa amemeza kete 82
aina ya heroini zilizokuwa zimefungwa kwenye karatasi zinazofanana na
ganda la sigara, ambazo si rahisi kuonekana katika mitambo.
Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkuu wa
Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Alfred Nzowa zimesema pamoja
na mbinu zake na kujiamini, mwanamke huyo alikamatwa kutokana na
ushirikiano wa vitengo mbalimbali vya uwanja wa ndege.
No comments: