Ads Top

KATIBU MKUU WA CCM, KINANA AMALIZA ZIARA YAKE WILAYANI NZEGA, LEO NDANI YA WILAYA YA UYUI MKOANI TABORA

 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Taifa Kata ya Bukene, wilayani Nzega, wakati wa mwendelezo wa ziara hiyo ndani ya  Mkoa wa Tabora.Kinana amemaliza ziara yake katika Wilaya ya Igunga na Nzega na kesho kuhamia wilayani Uyui,katika suala zima la kuimarisha chama,kutekeleza na kuhimiza maendeleo ya Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010,sambamban a kusikiliza matatizo ya wananchi na kuyapatia ufumbuni kwa namna moja ama nyingine,zira hiyo itakuwa ni ya siku kumi ndani ya mkoa wa Tabora.
Baadhi ya wakazi wa jimbo la Bukene wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa,kata ya  Bukene, wilayani Nzega

Wanachama wapya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakila kiapo cha utii cha chama hicho, baada ya kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa katika Kata ya Bukene, wilayani Nzega leo.
Katibu wa NEC,Uenezi siasa na Itikadi,Nape Nnayue akiwahutubia wakazi wa Bukene,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Taifa Kata ya Bukene, wilayani Nzega, mkoani Tabora.
Baadhi ya wakazi wa jimbo la Bukene wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa,kata ya  Bukene, wilayani Nzega
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye wakiwapungia mikono wananchi baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa katika Kata ya Bukene, wilayani Nzega
Kinana akishiriki kufyatua tofali ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mradi wa matofali wa akina mama wa CCM Wilaya ya Nzega. Mradi huo umefadhiliwa na Mbunge wa Viti MaalumMkoa wa Tabora, Munde Tambwe (pichani kushoto), katika eneo la Ofisi za CCM Wilaya ya Nzega .
 Kinana akiwa na Mohamed Kashindye mmiliki wa shamba la kumwagilia la mpunga  alipoombwa kwenda kulikagua,katika Jimbo la Bukene, wilayani Nzega. Mkulima huyo alimuomba Kinana kufanya hivyo licha ya shamba lake kutokuwemo kwenye ratiba ya ziara ya kiongozi huyo. Kinana alikubali kukagua shamba hilo na kumpongeza Kashindye kwa kilimo hicho.
 Kinana akishuka kwenye tanki  alipokuwa akikagua mradi wa maji wa Kijiji cha Itobo, Jimbo la Bukene, wilayani Nzega
Kinana akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Taka Nzega, Samweli Buyigi alipokuwa akikagua chujio la maji mjini Nzega
Wananchi wakifautilia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Itobo,jimbo la Bukene wilani Nzega mkoani Tabora.
 Vijana wakitumbuiza kwa ngoma ya zeze walipokuwa wakimlaki Kinana katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Itobo, Jimbo la Bukene.
Wananchi wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu Kinana akihutubia katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Itobo. 
 Nape akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Itobo.
 Sehemu ya umati wa watu uliofurika kwenye mkutano wa CCM Kata ya Bukene .
Kinana akihutubia katika mkutano huo na kukemea kitendo cha wana Ukawa kuwatukana vingozi waasisi wa muungano.
Kinana akikagua mradi wa maji ndani ya jimbo la Bukene,wilayani Nzega mkoani Tabora.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.