KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS-IKULU: MAKAMU WA RAIS DKT. BILA AFUNGUA MKUTANO WA TATU WA BARAZA LA MAWAZIRI WA NCHI ZA MAZIWA MAKUU NA NCHI MAJIRANI ZA UMOJA WA KUDHIBITI SILAHA NDOGO (RECSA).

Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima, akizungumza wakati wa mkutano huo
kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais kufungua mkutano huo.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akihutubia wakati akifungua rasmi Mkutano Maalum wa tatu wa Baraza la
Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Nchi Majirani zinazounda Umoja wa
kudhibiti Silaha ndogo (RECSA), uliofanyika leo mchana kwenye Hoteli ya
Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam. Umoja huo unaundwa na nchi 15
ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Somalia,
Sudan, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Shelisheli,
ElitreaAfrika ya Kusini, Jibuti na Afrika ya Kati.

Baadhi
ya wadau na washiriki wa mkutano huo, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt.
Bilal, wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa Mkutano huo leo kwenye
Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na baadhi ya washiriki wa
mkutano huo baada ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano huo.

akiagana na baadhi ya viongozi wa wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za
Maziwa Makuu na Nchi Majirani zinazounda Umoja wa kudhibiti Silaha ndogo
(RECSA), baada ya kufungua rasmi mkutano huo leo kwenye Hoteli ya Hyatt
Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.Ofisi ya Makamu wa Rais
No comments: