Mvua yaleta kizaazaa jijini Mwanza
Baadhi ya
magari yaliyozingirwa na maji katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza baada
ya Mvua kubwa kunyesha julai 26 mwaka huu. Picha na
Antony Sollo
Na Antony
Sollo Mwanza
Julai 26
2014.
Mvua iliyonyesha julai 26 jijini Mwanza imeleta
kizaazaa na kusababisha Mkutano wa Naibu katibu Mkuu wa chama cha mapinduzi
mwigulu Nchemba kuingia dosari,mvua hiyo iliyoanza kunyesha majira ya saa tatu
asubuhi hadi saa saba mchana,imesababisha taharuki kubwa kwa wakazi wa jiji la
Mwanza na Vitongoji vyake hii ni baada ya maji kujaa na kusababisha baadhi ya
barabara kukatika na kusababisha usafiri kuwa wa shida jijini humo.
Wakizungumza na Tanzania Daima, wananchi
waliokuwa jirani na uwanja huo, walisema mvua hiyo haijawahi kunyesha kwa
kipindi chote cha masika kwa msimu wa 2014.
Mvua hiyo pia imesababisha baadhi ya mabomba ya
maji katika uwanja wa CCM Kirumba kupasuka na kusababisha huduma mbalimbali
kukwama.
Akizungumzia mazingira ya uwanja wa CCM Dereva
mmoja wa gari la Chama cha Mapinduzi aliyesema kuwa hatapenda kuandikwa
gazetini alishangazwa na kuanza kutoka maji katika uwanja huo jambo ambalo si
la kawaida kufuatia kukatwa kwa maji katika Uwanja huo baada ya wamilki wa
uwanja huo kushindwa kulipa bili za maji.
“Au kwa kuwa Naibu Waziri yuko hapa ndiyo
kasababisha maji haya yatoke? alihoji Abdalla Nasoro ambaye ni mmojs wa wanachama
wa CCM”
No comments: