Ads Top

Kutoka IKULU: Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete Alipowasili na Kuoongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mjini Dodoma

 Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba Mhe Samwel Sitta alioowasili kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM Dodoma Agosti 19, 2014. Kulia ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora), Mhe George Mkuchika
 Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais  Jakaya Mrisho Kikweteakiagana na wajumbe wa Kamati  Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mbunge wa Songea mjini Dkt Emmanuel Nchimbi, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na  Mbunge wa jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagama, na Naibu Waziri wa Fedha na mbunge wa Iramba Magharibi Mhe Mwigulu Nchemba 
 Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa katika Uwanja wa ndege wa Dodoma na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Dkt Emmanuel Nchimbi
Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM Dodoma Agosti 19, 2014. Kushoto ni Makamu wa Mwenyekiti wa CCM (Visiwani) na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein. Kulia ni Makamu wa CCM (Bara) Ndg Philip Mangula akifuatiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana.Picha na IKULU

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.