Mamia ya watu kwa shangwe na vigelegele wamemkaribisha Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta baada ya kurejea kutoka kikao chake katika mahakama ya kimataifa ya ICC mjini the Hague
Kenyatta alihudhuria kikao maalum katika mahakama hiyo Jumatano, na
kuwa Rais wa kwanza aliye mamlakani kufika katika mahakama hiyo.
Mahakama
hiyo ilimtaka afike mbele yake kutokana na malalalmsihi kutoak kwa
kiongozi w amashitkaka kuwa serikali ya Kenya inaficha ushahihidi
kuhusiana na kesi inayomkabili.
Alikanusha madai ya uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa ghasia za
baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007 ambayo yalisababisha vifo vya
watu 1,200 na kuwaacha wengine zaidi ya laki sita bila makao.
Kenyatta alipokelewa na idadi kubwa ya watu waliokuwa wanacheza densi pamoja na gwaridde la heshima.
Asubuhi na mapema, wafuasi wake walipanga foleni kwenye barabara ya kutoka uwanja wa kimataifa wa ndege mjini Nairobi.
Walipeperusha bendera na kusikika wakiimbia kwa shangwe na kumsifgu Kenyatta wakisema kuwa Rais wao hana hatia.
Rais aliwahutubia kwa mda mfupi umati huo wa watu ambao waliombwa kufika kumpokea rais na waziri wa usalama.
Mwandishi wa BBC aliyefika kushuhudia Rais huyo akiwasili nchini alisema kuwa Kenyatta ana wafasui wengi.
Habari na BBCswahil.com
No comments: