Ads Top

Tazama jinsi Katiba Ilivyo kabidhiwa kwa Rais wa Tanzania Bara Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dr Ali Shein

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akipokea Katiba Inayopendekezwa toka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta wakati wa sherehe ya Makabidhiano ya Katiba hiyo iliyofanyika jana 8 Oktoba, 2014 mjini Dodoma.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein (kushoto) akipokea Katiba Inayopendekezwa toka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta wakati wa sherehe ya Makabidhiano ya Katiba hiyo iliyofanyika jana 08 Oktoba, 2014 mjini Dodoma.

Marais wote wa Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakikata utepe kufungua Katiba Inayopendekezwa wakati wa sherehe ya makabidhiano ya Katiba hiyo hapo jana 8 Oktoba, 2014 mjini Dodoma.
Marais wote wa Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakionyesha juu Katiba Inayopendekezwa ili wananchi waweze kuziona wakati wa sherehe ya makabidhiano ya Katiba hiyo hapo jana 8 Oktoba, 2014 mjini Dodoma.
Marais wote wa Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakionyesha nyuso zenye furaha mara baada ya kukabdihiwa rasmi Katiba Inayopendekezwa wakati wa sherehe ya makabidhiano ya Katiba hiyo hapo jana 8 Oktoba, 2014 mjini Dodoma.
Alyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Andrew Chenge akitoa hotuba mbele ya Marais wa Tanzania Bara na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na wananchi waliohudhuria wakati wa sherehe ya Makabidhiano ya Katiba Inayopendekezwa siku ya tarehe 8 Oktoba, 2014 mjini Dodoma.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba. Mhe. Samuel Sitta akitoa hotuba mbele ya Marais wa Tanzania Bara na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na wananchi waliohudhuria wakati wa sherehe ya Makabidhiano ya Katiba Inayopendekezwa siku ya tarehe 8 Oktoba, 2014 mjini Dodoma.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein akiwahutubia wananchi pamoja na wageni waalikwa wakati wa sherehe ya Makabidhiano ya Katiba Inayopendekezwa siku ya tarehe 8 Oktoba, 2014 mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wananchi pamoja na wageni waalikwa wakati wa sherehe ya Makabidhiano ya Katiba Inayopendekezwa siku ya tarehe 8 Oktoba, 2014 mjini Dodoma.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akipokea Cheti cha heshima ya uongozi toka kwa Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya, wakati wa sherehe ya makabidhiano ya Katiba hiyo hapo jana 8 Oktoba, 2014 mjini Dodoma.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akionyesha juu Cheti cha heshima ya uongozi mara baada ya kukabidhiwa toka kwa Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa sherehe ya makabidhiano ya Katiba hiyo hapo jana 8 Oktoba, 2014 mjini Dodoma.
Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha akipokea Cheti cha heshima ya uongozi toka kwa Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa sherehe ya makabidhiano ya Katiba hiyo hapo jana 8 Oktoba, 2014 mjini Dodoma.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.