Mwanamke mmoja nchini Marekani amejifungua mtoto mwenye uzito wa paundi 14.1 sawa na kilo 6.4kg na sasa mtoto huyo anakula mara mbili zaidi ya uwezo wa mtoto mchanga
Avery mtoto mkubwa kuliko kawaida nchini Marekani
BiMaxxzandra Ford amepata mtoto aliyempa jina Avery, ndiye mtoto
mkubwa na mzito kuwahi kuzaliwa katika hospitali ya wanawake ya
mtakatifu Joseph iliyoko Tampa, Florida.Avery, alizaliwa kwa njia ya
kawaida .
Ford alikuwa hajatanabahi kuwa yu mjamzito mpaka
alipotimiza wiki 35 .lakini mara baada ya kuwa anaongezeka uzito kupita
kiasi ,madaktari wakamthibitishia kuwa yu mja mzito,na kutokana na kasi
ya unenepaji mwanzo Bi Ford alihisi atajifungua watoto pacha,kumbe
sivyo.
Debbie Moore, mkunga katika hospitali hiyo, wasingemruhusu
mwanamke huyo ajifungue kwa njia ya kawaida kama wangegundua mapema ana
mtoto mwenye kilo nyingi kiasi hicho .
Avery anabaki hospitalini
chini ya uangalizi maalumu tangu alipozaliwa tarehe 29 January , lakini
anatarajiwa kuruhusiwa kwenda nyumbani hivi karibuni.
Bi Ford, anaye mtoto mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja na mtoto wa kike mwenye miaka mitano.
habari na BBCswahil.com
No comments: