MTU MMOJA AFARIKI KATIKA AJALI YA GARI NA 4 WAMEJERUHIWA AKIWEMO MAMA TUNU PINDA MOROGORO.
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa akiwemo mke
wa waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda Mama Tunu Pinda baada ya gari
walilokuwa wakisafiria kumgonga mwendesha pikipiki wakati akikatisha
barabara katika eneo la Mkundi barabara ya Morogoro Dodoma manispaa ya
Morogoro.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa nane mchana katika eneo la Mkundi
ikihusisha gari lenye namba za usajili STK 9242 gari la mke wa waziri
mstaafu Mizengo Pinda likitokea Dodoma kwenda jijini Dar-es-Salaam na
pikipiki ambapo mkuu wa mkoa wa Morogoro Dokta Rajabu Rutengwe anaelezea
kuhusiana na ajali hiyo.
Majeruhi wengine wa ajali hiyo ni dereva wa gari hilo Bw Anjelo
Mwisa, mlinzi wa mke wa waziri mkuu mstaafu Gaudensi Tembo na kijana wa
familia ya Mama Tunu Pinda Bwana Gilbert Sampa.
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoa wa
Morogoro Dr Rita Liamuya amesema hali ya mke wa waziri mkuu mstaafu na
majeruhi wengine zinaendelea vizuri na kueleza kuwa majeruhi hao
wanatarajia kuhamishiwa jijini Dar-es-Salaam kwa matibabu zaidi.
No comments: