Ads Top

WIZARA YA FEDHA IMEIPATIA IDARA YA MAHAKAMA SH BILIONI 12.3 KUBORESHA UTENDAJI KAZI.

Wizara ya fedha imetimiza ahadi ya rais Dr. John Magufuli aliyotoa siku nne zilizopita kwa idara ya mahakama wa kuipatia idara hiyo shilingi bilioni 12.3 ili ziweze kusaidia uendeshaji wa mahakama nchini hasa usikilizaji wa kesi zinazohusiana na kodi.

Fedha hizo zimekabidhiwa kwa idara ya mahakama na waziri wa fedha na mipango Dr.Philip Mpango ambapo amesema serikali inatumaini utendaji kazi wa mahakama sasa utafanyika kwa kasi zaidi.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.