RAIS DKT.MAGUFULI AMESEMA KUWA HATOINGILIA MGOGORO WA UCHAGUZI ZANZIBAR.
Rais Dakta.John Pombe Magufuli amesema hataingilia mgogoroo wa Zanzibar na kuwataka wenye malalamiko waende mahakamani.
Akiongea na wazeee wa mkoa wa Dar es Salaam rais Magufuli amesema
katiba ya Zanzibar imeweka uhuru wa tume ya uchaguzi kama ilivyo tume
ya uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano na hivyo kama kiongozi anayeheshimu
utawala wa sheria hawezi kuingilia suala hilo.
Dakta.Magufuli ambaye hii ni mara yake ya kwanza kuongea na wazee
wa Dar es Salam tangu kuingia madarakani ameomba watanzania kuiunga
mkono serikali ya awamu ya tano katika kudhibiti wabadhirifu ili
kuelekeza fedha zitakazopatikana kwenye mipango ya maedneleo nakuapa
kutovumilia wala rushwa na wazembe huku akionya wanaokejeli kuwa kasii
yake ni nguvu ya soda.
Kuhusu michango rais amesema katika elimu michango yote ni hiari na
kwamba wakuu wa mikoa na wilaya watapimwa kwa kadiri wanavyotekeleza
wajibu wao kwa kutatua kero za wananchi ikiwemo kero ya madawati.
Rais hakuacha kusisitiza watanzania wazalendo kutumia fursa ya
serikali ya awamu ya tano kuwekeza katika nchi yao kwa kadiri
wanavyoweza.
Tanzanian Shilling Converter
No comments: