WAKAZI WA KIJIJI CHA LASHAINI MONDULI WALALA NJE BAADA YA KUBOMOLEWA NYUMBA ZAO
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Lashaini wilaya ya Monduli Mkoani
Arusha hawana mahali pa kuishi na wamelazimika kulala nje baada ya
nyumba zao kubomolewa kwa madai ya kujenga katika eneo linalodaiwa kuwa
ni la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWT).
Wakizungumza na ITV iliyo fika katika eneo hilo na kujionea hali
halisi huku baadhi ya watoto na wanawake wakiwa wameketi katika vitanda
vilivyo njee baada ya nyumba kubomolewa na kudai kuwa wapo kwenye
maeneo halali na waliiomba serikali ipeleke kipimo cha GPS kama ilivyo
ahidi mwaka jana ili kuhakiki maeneo hayo lakini hadi sasa haijapeleka
watalam na kwamba wakigundulika wapo ndani ya eneo la jeshi wapo tayari
kuondoka lakini hada sasa wanaimani awajavuka nje ya maeneo yao halali.
Afisa ardhi wa wilaya ya Monduli Abili Mwanga amesema kimsingi
wananchi wamejenga nje ya eneo linalo milikiwa na jeshi na kwamba
wamebolewa kimakosa na hata litakapo pimwa kwa bado eneo hilo litakuwa
nje ya eneo linalodaiwa.
Akizungumza baada ya kutembelea nyumba zilizo bomolewa mkuu wa
wilaya ya Monduli Francis Miti amesema amezungumza na viongozi wa jeshi
na kumpa maelezo kwanini wamevunja nyumba hizo lakini mazungumzo ya
kina yatafanyika juma tatu ili kupata ufumbuzi wa mgogoro huo kabla ya
kuleta madhara zaidi.
No comments: