NYOTA WA TAARAB MARIAM HAMIS ‘PAKA MAPEPE’ KUZIKWA LEO
Sehemu ya wanawake waliofika kwenye msiba.
MWIMBAJI mahiri wa taarab nchini Mariam Hamis ambaye amefariki jana alfajiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matatizo ya uzazi, atazikwa leo saa kumi jioni katika makaburi ya Magomeni Fundikira.
Mariamu ambaye alitamba na wimbo wa Paka Mapepe ambao aliuimba akiwa katika bendi ya East African Melody mpaka umauti unamkuta, alikuwa mwanamuziki wa bendi ya TOT taarab ambayo alijiunga mwaka juzi akitokea katika bendi ya Five Stars.
No comments: