RE: SERIKALI HAINA NIA MBAYA KUONDOA CHANNEL KWENYE VING'AMUZI
Na Antony Sollo Geita.
SERIKALI kupitia Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini imetoa ufafanuzi juu ya malalamiko yaliyoibuka toka kwa watumiaji wa vinag’amuzi vya Multchoice- DSTV, Zuku na Azam kuhusu kutakiwa kuondoa channel za Televisheni zinazotazamwa bila malipo ikiwemo Channel Ten, Itv, Clouds Tv, na EATV.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Geita Mhandisi James Kilaba alisema hatua hiyo imechukuliwa ikiwa ni kulinda sheria na taratibu ambazo mamlaka ya mawasilino Tanzania ambayo TCRA ndio watekelezaji akiwataka kila mwenye leseni kuheshimu Sheria na kiwahimiza wananchi kutumia ving’amuzi sahihi ili kupata huduma za maudhui ya bila malipo yaani Free to Air – FTA.
Mhandisi Kilaba alisema kuwa vyombo vya habari vilivyotajwa hapo juu vilitoa tamko la maoni yao kuhusu kadhia hiyo na kubainisha kuwa licha ya kwamba sheria ilivunjwa haiwezi kuendelea kuvunjwa.
Ingawa hayo yote yamefanyika kwa takribani miaka miwili Serikali iko tayari kupoka maombi ya wamiliki wa leseni hizo ili wapate kibali na waweze kulipa kodi.
Pamoja na mapendekezo ya wamiliki hao kulipeleka jambo hili bungeni ili kubadili sheria Serikali haiko tayari kuacha Sheria ziendelee kuvunjwa.
Akijibu swali kutoka kwa mwandishi wa habari juu ya baadhi ya hatua zitakazochukuliwa dhidi ya wamiliki wa leseni waliopewa leseni ya kuonyesha channel hizo bila malipo kutofanya hivyo Mhandisi Kilaba alisema tayari suala hilo linafanyiwa kazi na matokeo yake yatakuja kuonekana siku si nyingi.
Hata hivyo Kilaba alisema, wananchi waelewe kuwa Serikali ya awamu ya tano inayo nia ya dhati kuhakikisha wanapata Habari lakini Sheria iwalinde na kama kuna chaneli zilitakiwa kuonekana kiwilaya zitimize takwa hilo la kisheria
“Naomba sana wananchi waelewe kuwa Serikali ya awamu ya tano inayo nia ya dhati kuhakikisha wanapata Habari lakini Sheria iwalinde na kama kuna chaneli zilitakiwa kuonekana kiwilaya zitimize takwa hilo la kisheria na kama ni za Mkoa na Kitaifa zinapashwa kuheshimu Sheria kwa mujibu wa leseni waliyoomba”alisema Kilaba.
Mwaka 2012 Tanzania ilizima rasmi mitambo ya analojia na kuingia kwenye mfumo wa digitali ambapo ving’amuzi vinne vilishinda zabuni ya kuonyesha channel tano za kitaifa bure ambavyo ndivyo vinaruhusiwa kufanya hivyo pekee na kilichotokea sasa ni ving’amuzi visivyokuwa na leseni hiyo kuonyesha pia channel hizo.
MWISHO

No comments: