Ads Top

ALIYEJIFANYA MWANDISHI WA BBC AWALIZA MAWAKALA ITV


MWANDISHI Tapeli aliyewahi kutiwa hatiani na Hakimu wa Mahakama ya
Mwanzo ya Wilaya ya Kahama,Mkoani Shinyanga sept 14, 2017Chrispin
Kilima ( 25 ) mwenyeji wa Mkoa wa Arusha kwa kosa la kujifanya
mwandishi wa habari wa Voice of America na kutumia jina la Igunza
Emmanul ametokomea kusikojulikana huku akiondoka na vifaa mbalimbali
mali ya Wakala wa ITV na Clouds TV kanda ya ziwa yenye makao yake
Mkoani Geita Tanzania Daima linaripoti.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu mmoja wa Wakurugenzi wa
Kampuni ya Mwana Leonard Co Ltd Leonard Paul alisema kuwa julai mwaka
huu Kilima alifika Ofisini hapo akiomba kuwa mmoja wa wafanyakazi wa
Kampuni hiyo akijitambulisha kuwa ni mtaalamu wa masuala ya Kompyuta.

Kwa mujibu wa Paul Kilima alifanyiwa usaili na kupatiwa nafasi hiyo
ambapo baada ya kukaa kazini kwa takribani siku tano alitoa taarifa
kuwa amepata kazi ya kwenda kufanya matangazo na taasisi moja mjini
Geita ambapo aliomba vifaa vya kufanyia kazi na kukabidhiwa Video
Camera aina ya Sony HD yenye thamani ya Shilingi mil3.5 pamoja na
Kamera aina ya Nikon D3400 yenye thamani ya Shilingi Mil 1.5.vyote
vikiwa na thamani ya Shilingi Mil 5.

Hata hivyo taarifa zingine ambazo zimelifikia gazeti hili zimeeleza
kuwa Kilima alitotoka na vifaa mbalimbali mali ya Wakala wa ITV na
Clouds TV zikiwemo Laptop mbili ambazo haikufahamika mara moja aina na
thamani ya Kompyuta hizo.

Katika hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Mwanzo Kahama mbele ya
Hakimu mfawidhi wa Mahakama hiyo Edina Sospeter ,Kilima alikuwa
akikabiliwa na Mashtaka ya wizi na utepali wa Laptop  na begi la
mwandishi wa Habari Patrick Mabula  wa gazeti la Majira.

Akitoa hukumu hiyo mwaka 2017 Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Edina
Sospeter alisema ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka kuwa
Kilima alijifanya mwandishi wa habari wa VoA na kutapeli laptop na
begi pamoja na flashi Disck aliyokuwanayo mtoto wa Patrick , Emmanuel
Patrick ulikuwa ni wa kweli na usiotia shaka hivyo Mahakama hiyo
kumtia hatiani mshtakiwa kwenda jela miezi minne au kulipa faini ya
sh.100,000.

Katika hukuma hiyo Hakimu Sospeter alisema ushahidi uliotolewa na
mtoto Emmanuel Patrick kuwa agosti 21 majira  ya saa moja na nusu
usiku mtuhumiwa  akiwa anajitambulisha kwa kutumia jina lisilokuwa la
kwake la  Igunza Emmanuel  alitapeli laptop ya Patrick  katika ofisi
yake baada ya kumrumbuni mtoto wake Emmanuel kisha kutoweka nayo na
kuiuza katika wilaya ya Segerema.

Mbele ya mahakama hiyo hakimu Sospeter kwa kuzingatia ushahidi
uliotolewa na shahidi wa pili wa upande wa mlalamikaji Paul Kayanda
ambae ni mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru pasipo shaka kuwa
Kilima alijifanya mwandishi wa habari wa Voice of America na kupeli
laptop hiyo kwa Emmanuel.

Hakimu Sospeter alisema Kilima baada ya kutapeli laptop hiyo alikwenda
kuiuza wilayani Segerema  mkoa wa Mwanza kwa kiasi cha Sh.350,000 na
kisha kukimbilia wilayani Chato alikokamatwa na polisi na kuletwa
wilayani Kahama kujibu kesi hiyo.

Alisema utetezi   uliotolewa na Mshitakiwa mbele ya Mahakama hiyo
ulikuwa ni wa kuidanganya kwa hiyo ameamua kumpatia adhabu hiyo ili
liwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia hiyo ya kufanya makosa ya
jinai .

Hakimu Sospeter alisema Mahakama imeridhika pasipo kuacha shaka na
ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka na  mashahidi  Kayanda na
Joseph Patrick  kuwa mshitakiwa Kilima aliiba laptop hiyo na
kumuhukumu kwenda jela miezi minne au kulipa faini ya sh.100,000
lakini alishindwa kutoa faini hiyo na kwenda jela.

Wakiongea kwa nyakati mbalimbali baada ya hukumu hiyo  wadau wa habari
wilayani Kahama walisema Kilima amekuwa akijifanya mwandishi wa habari
wa vyombo mbali mbali vya nje ya nchi na ndani ya nchi na kutumia
majina yao kisha kufanya utapeli wa vifaa vyao kama kamera, laptop ,
fedha na mabegi jambo linaloidhalilisha taaluma ya Habari nchini.

Naye Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Shinyanga
(SPC ) Kadama Malunde aliipongeza Mahakama ya Mwanzo Wilaya ya Kahama
kwa  adhabu hiyo na kutoa wito kwa waandishi wa habari  kupiga vita
vitendo vya watu ambao wamekuwa wakijifanya wanahabari na kuchafua
tasinia hiyo na wanapowabaini wenye tabia hiyo kuwalipoti katika
vyombo vya dola.

Hata hivyo Tanzania Daima lilimtafuta kwa njia ya simu ya kiganjani
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Katavi Walter
Mguluchuma ambaye alisema Kilima alikuwa amefanya utapeli  kama huo
wa vifaa mbalimbali Mkoani hapo kwa kujifanya Mwandishi wa habari na
mtoto wa Seleman Kova  na walishafungua jalada lenye namba
MPD/RB/840/2017 na alikuwa anatafutwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya
wizi.

Baada ya hukumu hiyo Wilayani Kahama Jeshi la Polisi kutoka Mkoani
Katavi lilifika na kumchukua kilima baada ya waandishi wa Habari
kulimpia faini ili apelekwe Mpanda Mkoani Katavi kwa ajili ya kesi
iliyokuwa imefunguliwa ambapo alitiwa hatiani na Mahakama ya Mwanzo
Mpanda kwenda jela mwaka mmoja na baadaye aliachiwa kwa msamaha wa
Rais April mwaka huu.

Kwa mujibu wa uongozi wa Wakala wa ITV na Clouds TV kanda ya ziwa
mshirika wa Kilima ambaye jina lake halikufahamika mara moja tayari
ametiwa mbaroni na Jeshi la Polisi Wilayani Sengerema akiendelea
kuhojiwa juu ya tuhuma za utapeli wanaofanya kwa ushirikiano na
mtuhumiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza Ahmed Msangi alipotafutwa kwa njia ya
simu kuzungumzia tukio hilo simu yake ilipokelewa na msaidizi wake
ambaye alisema kuwa Kamanda Msangi alikuwa kwenye msafara wa Waziri wa
Miundombinu kwa ajili ya shughuli za uzinduzi wa kivuko kipya.
MWISHO.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.